Mchezaji wa timu ya TSN, Sodi Ahmed (kulia) akimramba chenga Abdallah Fundi, wa timu ya Free Media, wakati wa mchezo wa michuano ya Kombe la NSSF 2013, uliochezwa leo asubuhi kwenye Uwanja wa TCC Chang'ombe jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo timu ya TSN imeibuka na ushindi wa mabao 5-0, mabao hayo yakiwekwa kimiani na wachezaji, Rashid Kagusa, aliyesalimia nyavu mara tatu, Evance Samwel, aliyefunga bao 1 na Said Kabasha, aliyetupia bao 1.
 Beki wa TSN, Sufianimafoto (kushoto) akichuana kuwania mpira na mshambuliaji wa Free Medi, saleh Ally, wakati wa mchezo huo.
 Mshambuliaji wa Free Media, Saleh Ally (katikati) akijaribu kuwatoka mabeki wa TSN, wakati wa mchezo huo.
Kwa picha zaidi bofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...