Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bibi Rehema Madenge akifunga rasmi mkutano kati ya Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma na Wakurugenzi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa uliomalizika mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa St. Gaspar mkoani Dodoma.
Wakurugenzi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa wakimsikiliza Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Bibi Rehema Madenge alipokuwa akifunga rasmi mkutano kati ya Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma na Wakurugenzi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa mwishoni mwa wiki katika ukumbi wa St. Gaspar mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma (kushoto) Bwana Vincent Mrisho akiteta jambo na Katibu wa Bodi hiyo Bibi Tamika Mwakahesya (kulia) wakati wa mkutano wa siku mbili kati ya Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma na Wakurugenzi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa uliofanyika tarehe 21-22 Machi katika ukumbi wa St. Gaspar mkoani Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma (aliyevaa suti kulia) Bwana Vincent Mrisho akiteta jambo na Katibu wa Bodi hiyo Bibi Tamika Mwakahesya (aliyeshika begi) na baadhi ya wajumbe wa mkutano kati ya Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma na Wakurugenzi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa uliofanyika tarehe 21-22 Machi katika ukumbi wa St. Gaspar mkoani Dodoma.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bibi Rehema Madenge aliyevaa vitenge (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Mishahara na Masilahi katika Utumishi wa Umma Bwana Vincent Mrisho (kulia) na Katibu wa Bodi hiyo Bibi Tamika Mwakahesya (kushoto) pamoja na baadhi ya Wakurugenzi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa uliofanyika tarehe 21-22 Machi katika ukumbi wa St. Gaspar mkoani Dodoma.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...