Meneja Mkuu wa Global Publishers, Abdallah Mrisho (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani). Kulia ni Meneja wa TMK Wanaume Family, Said Fella ‘Mkubwa’ na Meneja wa Wanaume Halisi, Abdallah Mashoto.
Mrisho akiteta jambo na Juma Nature na wenzake.
Wanaume Halisi wakiwa katika picha ya pamoja na meneja wao, Mashoto.
Wanaume Family wakiwa katika picha ya pamoja na meneja wao, Fella.
Juma Nature (kushoto) akiongea na waandishi wa habari.
Wasanii wa Wanaume Family, kutoka kushoto, Dogo Aslay, Stiko na YP wakiwa katika pozi.
Temba akiongea na waandishi wa habari.
Mhariri wa Gazeti la Risasi, Mohamed Kuyunga akiwa katika picha ya pamoja na Temba na Nature.
Temba akiingia kwenye gari lake tayari kwa kusepa.
Benjamin Mwanambuu, mmoja wa waratibu akiwa na Pamela Daffa, Mc wa dar Live.
Mashoto akitoa tambo zake.
Fella naye hakubaki nyuma, aliahidi makubwa.
Temba na wenzake wakisepa.
Ukumbi wa kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem, umeandaa mpambano wa kihistoria kati ya makundi mawili hasimu ya muziki wa kizazi kipya Bongo, TMK Wanaume Family na TMK Wanaume Halisi. Mpango mzima utatimua vumbi siku ya Pasaka na leo makundi hayo yalifanya mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi za Global Publishers, Bamaga jijini Dar.
Mjomba Michuzi,
ReplyDeleteMimi Mo Barron Mkazi wa Mbagala Kitaa ninaomba kazi ya Urefa, ama mnipe Kazi ya Mshika Kibendera wa Kulia ama Kushoto siku ya Mpambano huo wa Wanaume Family na Wanaume Halisi!!!
Haahidi yafuatayo:
1.Sintapokea Rushwa wala kupanga matokeo.
2.Nasema ukweli kwa kuwa mimi sitoke Temeke sio kwamba nakaa labda Mtaa wa Wailesi ama nipo Temeke Mwisho, ni Mkazi wa Mbagala kama nilivyo jitambulisha hapo juu hivyo sina upende wowote nitaegemea.
3.Naahidi kutoa FAIR PLAY!
Je, mtaninusuru vipi kwa Usalama wangu dhidi wa Mashabiki wakorofi?
Mtanipatia Glovu niwe kama Bondia?
Naweza kufanya Uamuzi huku nikiwa juu ya Dari la paa la jengo la Dar Live?