Mtoto Simon Mlope mwenye umri wa miaka 11 mkazi wa eneo la mahenge katika manispaa ya Songea mkoani Ruvuma alilazimika kukatisha masomo yake ya shule ya msingi akiwa darasa kwanza kutokana na mtoto huyo kusumbuliwa na ugonjwa wa moyo .

 Awali tulitoa habari za mtoto huyu akiomba msaada lakini hadi sasa bado hajapata msaada wowote ule wa kuweza kuokoa maisha yake. Nahivi sasa hali ya mtoto huyu inazidi kuwa mbaya kiafya .

Mtoto Simon Mlope alikubwa na ugonjwa huo wa moyo tangu mwaka 2001 mara baada ya kuzaliwa na kugundulika kuwa moyo wake una tundu hali ambayo inamsababishia mtoto huyo kuvuta pumzi kwa shida.

 Mama wa mtoto Simon Mlope anayeitwa AMINA ALLY anawaomba watanzania kumsaidia mtoto wake fedha za matibabu Baada ya kuambiwa na madaktari kuwa Simon anatakiwa kwenda nchini india kutibiwa,baada ya kupata rufaa kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili mwaka 2006 huku familia yake ikiwa haina uwezo kabisa.

Majirani wa familia ya Simon nao wanasema kuwa mtoto huyo anahitaji msaada wa haraka kwa kuwa hali yake sio nzuri na kuwaomba watanzania wamsaidie.

Kinachosikitisha zaidi baba wa mtoto huyo anayejulikana kwa jina la MLOPE ameondoka nyumbani hapo tangu mwaka 2011 na hajulikani aliko kwa sasa, ingawa mwanzoni alisema yuko nchini Msumbiji.

Kwa anayeguswa na tatizo hili na anataka kumsaidia SIMONI MLOPE atumie simu namba 

 0752732290
Mtoto Simon Mlope anavyoonekana hivi sasa kutokana na maradhi ya moyo yanayomsumbua.
Mtoto Simon Mlope akiwa na Mama yake Mzazi atambulikae kwa jina la Amina Ally.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. JAMANI TANGIA 2006 KWELI MPAKA LEO..KWANI MGONJWA AKIPEWA TRANSFAR NA HOSP YA SEREKALI NILIDHANI SEREKALI INATAKIWA KUMGARAMIA..EE MUNGU HEBUA WAPE AKILI ZA KUTOSHA VIONGOZI WETU

    ReplyDelete
  2. Eee mwenyezi Mungu mwenye kheri; waangazie hawa viongozi wetu wanaonunua magari ya kifahari badala ya kufikiria malaika kama hawa!
    Mithupu usiitupe kapuni ili wasome na kuangaziwa!!!

    ReplyDelete
  3. Nategemea LIONS CLUB ya Dar inawasaidia watu wenye matatizo ya moyo kuwapeleka India.Kinachoitajika ni kufuata utaratibu na kumchangia ili afike Dar kwa matibabu kisha serikali na Lions kumsaidia kwenda India

    ReplyDelete
  4. jamani muja wa kulaumiana siyo sasa, kwani haitasaidia. kama ni lawama basi wa kwanza ni jamii inayomzunguka huyo kijana, kwani hawakutoa ushirikiano kwa kukaa kimya, huyu kijana ang'etibiwa tangu 2006. basi yamesha tokea shime watanzania tukajitoa kuokoa maisha ya huyu kijana. lawama badaye. shime watanzania tujitoe kuokoa maisha ya huyu kijana taifa la kesho. asanteni.

    ReplyDelete
  5. Mungu ni mwema wakati wote, watanzania wote bila kujali itikadi zetu tumsaidie kijana huyu taifa la kesho. si wakati wa kutoa lawama kwa sasa tumsaidie kwanza. kama ni lawama basi ni kwa jamii inayomzunguka kwani tangu 2006 alimwona akiteseka ang'eshatibiwa muda.hivyo tuache malumbano tumsaidie. kutoa ni moyo na si ufisadi.

    ReplyDelete
  6. HAYA SHIDA NYINGINE INAJITOKEZA, MUHUSIKA AMETOA NAMBA YA SIMU MOJA TU. NIMEPIGA WEEEEEE IKO BIZ, MUDA TENA HAIPO HEWANI. SASA TUTAMSAIDIAJE? NAOMBA ANGALAU ATOE A/C YA BANK ITAKUWA RAHISI KUMSAIDIA. HATA KATIKA NUMBER ALIYOTOA HAWAJAELEZEA KAMA TUTUME KWA M-PESA AU LAA. ILA KWA M-PESA WAJANJA WANAWEZA TENGENEZA LAIN YA KITAPELI MUWE MACHO TAFADHALI.(MTOA MAONI NO.4)

    ReplyDelete
  7. Tumtumieni tu kwa Mpesa na kwa Wasiokua na namba yake, hii hapa 0752732290. Kutoa ni moyo si utajiri

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...