Kwa siku nzima ya leo, mawasiliano ya mtandao katika nchi za Afrika Mashariki yamepatwa na kwikwi kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni matatizo ya kiufundi yaliyoikumba mitambo ya kampuni ya Seacom, inayotoa huduma hiyo kwa njia ya mkongo upitao chini ya bahari.
Tayari Seacom, kupitia mtandao wake, imeomba radhi kwa kwikwi hiyo iliyosababisha tafrani kila mahali, ikiwemo Tanzania, na kuahidi kuirekebisha haraka iwezekanavyo.
Globu ya Jamii inaomba Kunradhi wadau kwa kukumbwa pia na kwikwi hiyo ambayo iko nje ya uwezo wetu. Tunaahidi kundeleza Libeneke mara tu mambo yatapotegamaa.
Kwa kuwa hii si kwikwi ya kwanza, tungependa kujua endapo kama hatua mbadala za makusudi zimewekwa ama zipo kukabiriana na kwikwi kama hii, ambayo kwa kweli inatoa raha kwa kukosesha wadau mawasiliano haya muhimu.
ANKAL
Tayari Seacom, kupitia mtandao wake, imeomba radhi kwa kwikwi hiyo iliyosababisha tafrani kila mahali, ikiwemo Tanzania, na kuahidi kuirekebisha haraka iwezekanavyo.
Globu ya Jamii inaomba Kunradhi wadau kwa kukumbwa pia na kwikwi hiyo ambayo iko nje ya uwezo wetu. Tunaahidi kundeleza Libeneke mara tu mambo yatapotegamaa.
Kwa kuwa hii si kwikwi ya kwanza, tungependa kujua endapo kama hatua mbadala za makusudi zimewekwa ama zipo kukabiriana na kwikwi kama hii, ambayo kwa kweli inatoa raha kwa kukosesha wadau mawasiliano haya muhimu.
ANKAL
Hawa jamaa waungwana kweli! Je TANESCO wakitaka kukata umeme au umeme ukikatika huwa wanawataarifu wateja wake au kuomba radhi pale umeme unapokatika?
ReplyDeleteAnkal Michuzi,
ReplyDeleteWaeleze hao jamaa 'Pull your socks' kwa kuwa wameshaingia mkenge kwa kusaini Mkataba na sisi hivyo wasiishie tu kutoa udhuru na samahani nyingiii wanatakiwa watubebe mgongoni!
Lazima waekewe sisi ni Wateja wakorofi, hatutaki kusikia vitu kama:
1-Suala lipo juu ya uwezo wetu,
:JE MLIPOSAINI MKATABA WA KUTOA HUDUMA MLIWEKA KIPENGELE HICHO?
2-Ohhh tumeghafirika,
:AFRIKA NDIO HAPA SASA MNAPOSEMA TUMEGHAFIRIKA TUWAPELEKE WAPI?, SAYARI INGINE?
3.Kutokana na sababu zisizoweza kuzuilika,
:WAJAMENI MMESOMA NA MKAELIMIKA KTK FANI, HIVI MLIPOKUWA MASOMONI PALIWAHI KUTOKEA SWALI LISILOKUWA NA JIBU?
Mjomba waeleze hao watu kuwa Michuzi Blogspot ina wateja wakorofi amabao hawawezi kustahimili kuwa disconnected kwqenye Libeneke!
Kama vipi wawe Ankali wanakulipa Fidia kwa sisi kukosa huduma ili wewe ufanye mpango wa 'kata mti panda mti' utafute njia mbadala ya kutumia wakati wa kwikwi zao!!!
Anonymous wa kwanza hapo juu hivi we unawapongeza hao jamaa na unasema ni waungwana kivipi?? Mbona nashindwa kukuelewa? kama ni mfuatiliaji wa huu mkonga mawasiliano utaona the way tunavyo hangaika punde huo mkonga unapopata technical fault. Anyway mimi lawama zangu kubwa ni kwa hawa TTCL ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa watoaji huduma za internet sehemu kubwa ya wananchi na mashirika hapa nchini, Nimekuwa nikiwapigia simu na kuwauliza why hii kitu inatokea kila siku?? majibu yao fibre imekatika huko Egypt na kama sikosei hii ni mara ya 3 sasa toka mwaka huu umeanza, nikiuliza tena why inakuwa hivi majibu ooh tunahujumiwa na baadhi ya makampuni ya simu ambayo hayajajiunga na mkonga wa mawasiliano hapa nchini hahaha come on guys hivi mnafikiri hii nchi bado kuna watu wa kufikirika?? Haya leo nikawachachamalia kuwa haiwezekani mwisho wa mwezi mkakata service zenu hata kama badi nina GB kadhaa zimebakia kwenye account yangu mana mmekuwa mkifanya hivyo bila kuwa na roho ya utu kama sie tunavyoweza kuwavumilia kukaa bila Internet kwa siku 3, majibu yakaja hii issue ni kubwa njoo ujaze claim form then tutakurudishia kha why tufanye vitu manualy? kwa nini nyie msitune vitu vyenu huko huko mi nisihangaike kuja huko ooh aaah ooh aah, haya na kwa nini hamna back up internet once kunapotokea matatizo kama watu wakaendelea kupata huduma? majibu unafikiri ni kitu rahisi? hahahaha Jamani huu mkonga wa mawasiliano si wajuzi tu kwani nyie si mlikuwa mnatumia satelite internet why mlizima hizo satelite zenu?? why msingeziacha na mkafanya kama back-up? majibu hilo ndo tunalotaka kulifanya sasa hivi mweh nikajichokea mie.......... Nakupenda Tanzania
ReplyDeleteWilly
TANESCO hawezi kuomba radhi kwa vile hata wao hawajui umeme wao wenyewe utakatika lini. Na kwa vile unakatika mara 4-8 kwa siku, siku 7 za juma, kuomba radhi mara 4-8 kwa siku, siku 7 kwa juma, itaonekana kama utani tu.
ReplyDeleteSEACOM ama sisi wenyewe tunahitaji plan B. Kukaa bila mtandao kwa dunia ya sasa si kitu kizuri. Mitambo ya benki, shule na vyuo, hospitali, jeshi, usalama nk katika karne hii inaendeshwa kwa mtandao. Kukosekana kwa mtandao is a security threat, economic threat, etc etc.
Hivi Kiswahili sawasawa ni 'mkongo wa taifa' au 'mkonga wa taifa'? ninavyojua mimi Mkongo ni mtu anaeoka DRC au Congo Brazaville. Na katika kamusi ya TUKI hakuna neno mkongo kwa maana hii iliyotumika katika kuharibika kwa mkongo. Isitoshe inaingia akilini kusema ni mkonga kwa maana ni matumizi ya kimithili yaani ile ni kama 'trunk'yaani mkonga wa tembo. Mimi nina wasiwasi kwamba hili neno mkongo limeingia katika lugha yetu kwa ajali ya istilahi na tahajia. Nadhani inawezekana kuna Mchina mmoja, wakati Huawei wanjenga Mkonga wa Taifa, alifanya kosa la kitahajia na basi toka hapo na sisi sote tunasema Mkongo wa Taifa na Mkongo wa SEACOM na kadhalika wakati tunapsawa kusema Mkonga wa Taifa na Mkonga wa SEACOM na kadhalika. Naomba tulifuatilie sana hili na TUKI na BAKITA na wengine tafadhali Michuzi.
ReplyDeleteMpeli