Kwa mujibu wa taarifa kutoka Kampala, Uganda, ni kwamba Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Afrika Mashariki wa Uganda Mhe Eriya Kategaya (pichani) amefariki dunia Jumamosi jioni katika Hospitali ya Nairobi, Kenya, alikokuwa amelazwa kwa takriban wiki moja kwa matatizo yaliyotajwa kitaalamu kama Thrombosis ambapo damu haizunguki vyema mwilini.
Tuungane na wana Afrika Mashariki wenzetu wa Uganda kuomboleza msiba wa Mheshimiwa huyu na kumuombea dua apate heri huko aendapo.
Mdau
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...