Katika kipindi cha Makutano kinachoendeshwa na Fina Mango wiki hii alifanya mahojiano na Miss Tanzania na Miss World Africa 2005, Nancy Sumari kuhusu mambo mbalimbali yanayomhusu katika maisha ya kabla na baada ya kutwaa mataji hayo makubwa na kuingia katika historia kama Miss Tanzania aliefanya vizuri zaidi kwenye mashindano ya ulimbwende duniani.

Nancy ambaye hivi karibuni amezindua kitabu cha watoto alichokipa jina la Nyota Yako alielezea nini hasa kilichomsukuma hadi kuamua kuandika kitabu hicho na kusema ilitokana na baada ya kuwa mama na kujikuta kila akienda maduka ya vitabu anakosa vitabu vya watoto vilivyoandikwa na waandishi wa Tanzania na kukuta vingi ni kutoka nje ya nchi, hivyo kuamua kuandika kitabu ambacho watoto wa kike wa Tanzania wataweza kukisoma na kuvutiwa kufanya kile ambacho muandishi amekielezea. “Kwa hivi sasa kitabu kinapatikana maduka ya Scholastica Mlinani City na pia Novel Idea Masaki na Ohio kwa shilingi 5,000 tu” alisema Nancy.

Lakini Nancy alikuwa na stori ya kusisimua kwani anasema kabla ya kuingia kwenye mashindano ya urembo alilazimika kufanya kazi kama muuzaji katika duka la fenicha kwa mshahara wa shilingi lakini moja na ishirini kwa mwezi. Hii ilitokana na kukwama kupata nafasi ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kitivo cha Sheria kutokana na chuo hicho kutoruhusu mwanafunzi aliemaliza kidato cha nne kwa elimu ya Kenya kujiunga moja kwa moja kwa ajili ya shahada.

Nancy amesema alifanya kazi hiyo kwa moyo wote hadi alipopata nafasi ya kushiriki taji la Miss Dar Indian Ocean baada ya kuonwa na wandaaji wa shindano hilo na kuibuka mshindi wa pili na baadae kuibuka Miss Kinondoni na hatimaye Miss Tanzania huku akisema kufanya kila kitu bila kuogopa kushindwa ndio siri hasa ya kufanikiwa licha ya kutokuwa na uzoefu wowote katika suala la urembo wa wakati huo na kusema hatimaye alifanikiwa kupata nafasi ya kuingia chuo kikuu cha Dar es salaam na atatarajia kumaliza masomo yake mwezi Julai.

Alipoulizwa nini ushauri wake kwa vijana wanaochipukia alisema “Let’s all try to become better people, everyone makes mistake no one is perfect lakini ni muhimu kama binadamu kujitahidi kufanya vitu sahihi sawa na unapoona ua linafifia linamwagilizie maji likue na unapomuona mwenzio anahitaji msaada na unayo nafasi ya kumsaidia usisite”

Mahojiano yote yanapatikana katika:


Muendeshaji wa kipindi cha Makutano Fina Mango akimsikiliza Nancy Sumari
Nancy Sumari akijibu moja ya maswali aliyoulizwa na Fina Mango

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. 120,000/= ni nyingi. Mimi wakati nasubiri kwenda chuo kikuu, nilifanyakazi iliyokuwa inanilipa 15,000/= kwa mwezi. Na nilikuwa sipewi yote mwisho wa mwezi ulipokuwa unafika. Nikiomba basi bosi anaingiza mkono mfukoni anatoa 3,000/= ananipa. Baada ya wiki hivi, ananipa 5,000/= hivi, kidogo kidogo hivyo mpaka 15,000/= inavyotimia. Ilikuwa haitoshi hata kwa nauli. Nauli wakati huo ilikuwa 100/= kwa trip. Kwenda na kurudi 200/=. Ofisi ilikuwa Kariakoo. Chakula cha mchana nilkuwa natumia 500/=. Baada ya kubakiza miezi 3 kujiunga chuo kikuu, niliamua kukaa nyumbani na kutiza TV badala ya kujisumbua na kazi.

    ReplyDelete
  2. Vitabu vya watoto mbona vipo vingi tuu sema hujazunguka madukani binti

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...