Na Shaffi Dauda
Hatimaye makamu mwenyekiti wa klabu ya Simba Godfrey Nyange Kaburu ametangaza rasmi kujiuzulu nafasi yake kwenye klabu ya Simba.
Taarifa rasmi kutoka kwenye uongozi wa Simba ni kwamba Kaburu leo ametuma barua pepe kwenda kwa mwenyekiti wa klabu ya Simba Mh.Aden Rage akimuelezea maamuzi yake ya kujivua madaraka ya kuitumikia Simba kutokana mgawanyiko mkubwa uliopo kwenye uongozi wa klabu hiyo.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari Kaburu ameelezea kwamba kamati ya utendaji imegawanyika na ufa uliopo hautoi nafasi nzuri kwake kuitumikia vizuri Simba, akisema ni moja ya sababu ya timu yao ya Simba kutofanya vizuri katika michuano mbalimbali inayoshiriki.
Pia Kaburu amesema amechukua maamuzi hayo ni njia mojawapo ya kuwajibika kama kiongozi kutokana mambo kutokwenda vizuri hali ambayo imesabababisha kutukanwa na kupigiwa kelele nyingi na wanachama na wapenzi wa Simba SC Mwenyekiti.
Hivyo ameamua kujiuzulu kupisha wanachama wengine wa Simba waweze kuliongoza jahazi la klabu hiyo.
Maji ya shingo!!!
ReplyDeleteHapa ndio pale unaposhuhudia Punda anakaa chini baada ya kuelemewa na mzigo mgongoni!
Duhhh huwezi amini na ngebe zake jamaa huyu mwenyewe anaachia ngazi?
Kaka kaburu nakupongeza sana tena sana kwa kuwa kama mtu umeshindwa kusimamia FAT mpaka mkafukuzwa je unaweza kuongoza hata familia yako?!
ReplyDeleteJamani mm kama shabiki wa Simba mambo sio kwa kweli. Embu atoke tuone asijekuja mtu mwinngine mwenye kuleta mabadiliko lakini sisi waTZ tuko after money sana hatuangaliagi Future. Alafu maneno mengi ka Kasuku.
ReplyDeletehapo hata kwa mangumi hakuna atakaye utaka uongozi wa msimbazi kwa sasa.
ReplyDeleteuongozi umekuwa ni kasa wa sumu!
hapo hata kwa mangumi hakuna atakaye utaka uongozi wa msimbazi kwa sasa.
ReplyDeleteuongozi umekuwa ni kasa wa sumu!
Ngoma inapokolea ni wakati Konga 'ngoma ndogo' zikirindima,,,na pale Msimbazi 'mibolo' imekolea Mabosi wa Timu wamechanganyikiwa mmoja baada ya mwingine wanaachia ngazi!
ReplyDeleteKaribu Yanga S.C tutakupa nafasi hiyohyio unayoiachia Msimbazi !!!
ReplyDeleteJe, ukivua hilo gwanda jekundu na ukivaa Kijani na Njano utaota mkia?
Nenda zako Yanga!
ReplyDeletePana uvumi unaosema uwa kwewe Kaburu ni mwana Jangwani!!!