Moshi mweupe umefuka katika  Sistine Chapel  leo jioni, kuashiria kwamba Papa mpya ameshachaguliwa na amekubali nafasi hiyo. Kwa mujibu wa kanuni za Kikatoliki, Bishop huyo mpya wa Rome anakuwa wa 266 na kuwa kiongozi wa kanisa Katoliki Duniani

Moshi huo mweupe umeonekana saa moja na dakika tano, baada ya raundi tano za kupiga kura. Papa Benedict wa XVI alichaguliwa katika siku ya pili baada ya raundi nne. 
Makadinali 115 walipiga kura kumchagua Papa mpya ambaye hadi dakika hii hajatambulishwa, na ili kuchaguliwa lazima atakuwa kapata kura angalau 77.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...