Mzee mzima  Carlos Santana ana ngoma nyingi kali kama hii ya 'Oye Como Va' ambayo enzi hizo kina Mesiaki walijifunzia kucheza cha cha cha pale YMCA. Watoto wadogo hata jina la wimbo hawaujui

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kweli wakati wa enzi za Ujamaa-halisi awamu ya kwanza vijana tulipata burudani za uhakika viwango vya kimataifa
    -kila mkoa au kanda kuna bendi ya muziki iwe Tabora, Moro, Dar, Iringa n.k
    - kumbi kibao za sinema miji yote ya Tanzania
    -timu za mpira wa miguu ambazo zilikuwa mabingwa wa ligi zao kama ya Uingereza zikiwa na wachezaji mahiri kama Martin Peters au Ujerumani mashariki walikuwa wanakuja sana Tanzania kucheza mechi wanja wa Taifa.
    - Bernhard (Berti)Carl Trautmann kipa mahiri wa Manchester City aliletwa Tanzania na kuwa kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars

    - disko la viwango vya kimataifa
    - usafiri DSM UDA kwa kutumia bus-pass unalipia mwezi mzima mbele
    - kumbi za usanii wa maigizo 'live' hii ikiwemo ngoma za kienyeji, michezo ya kuigiza kina Mzee Small live jukwaani n.k
    -gharama za maisha nafuu

    kama ni raha na burudhani vyote vilikuwa vya viwango vya kimataifa na original kweli kweli
    Mdau
    Kijana wa Zamani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...