Naibu Waziri Tamisemi(ELIMU) Ambae pia ni Mbunge wa Jimbo
la Ruangwa mkoani Lindi ,Kassim Majaliwa Akipokea msaada wa mashuka
100 kwa Mkurugenzi wa Masoko na Elimu kwa Umma toka Mfuko wa Taifa ya
Bima ya Afya(NHIF)Raphael Mwamoto kwa ajili ya vituo vya Afya vya
wilaya hiyo.
Mkurugenzi wa Masoko na Elimu kwa Umma toka Mfuko wa Taifa
ya Bima ya Afya(NHIF)Raphael Mwamoto akikabidhi mashuka 140 Diwani wa
kata ya Singino/Kivinje,Jafari Arobaini shuka ambazo zitasambazwa
katika vituo vya Afya vya wilaya hiyo.
Na Abdulaziz Video,Globu ya Jamii - Lindi
Imeelezwa kuwa Hospital ya Wilaya ya Kilwa/Kinyonga Mkoani Lindi
Inakabiliwa na Upungufu Mkubwa wa Shuka kwa ajili ya Wagonjwa
wanaolazwa katika Hospital hiyo pamoja na Vituo Vitano vya Afya
Wilayani humo.
Hayo yamebainishwa na Mganga mkuu wa Wilaya ya Kilwa Dr Mike Mabimbi
baada ya kukabidhiwa mashuka 140 na Mkurugenzi wa Masoko na Elimu kwa
Umma toka Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya(NHIF)Raphael Mwamoto katika
hafla fupi iliyofanyika katika hospital hiyo.
Amesema kwa sasa hospital yake yenye vitanda 90 kila kitanda kinatumia
mashuka mawili tu kwa siku ambayo hayakidhi mahitaji kwa mgonjwa
alielazwa ambae anapaswa kuwa na mashuka manne kwa siku
Dr Mabimbi amesema kupatikana kwa mashuka hayo kutasaidia baadhi
kusambazwa katika vituo vya Afya katika kata za
Tingi,Nanjirinji,Pande,Njinjo na Masoko ili kupunguza tatizo hilo sugu
kwa Wagonjwa.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mwamoto amesema msaada huo ni katika Juhudi
za Mfuko wake kuhakikisha kuwa Wagonjwa wanaolazwa hospitalini
wanapatiwa huduma Muhimu za Kijamii ikiwa ni pamoja na matibabu mazuri
.
Aidha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umekabidhi mashuka 100 kwa ajili
ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi katika Hafla fupi zilizofanyika
katika ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ruangwa na Hospital ya
Wilaya ya Kilwa(KINYONGA)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...