Benki ya NMB kwa kushirikiana na kampuni ya Fair Deal Auto Private Limited pamoja Car & General Ltd zinazosambaza pikipiki za miguu mitatu aina ya TVS King leo zimeingia ubia wa kutoa mikopo ya pikipiki za miguu mitatu aina ya Bajaaj na TVS King kwa bei nafuu zaidi. Pikipiki hizi zitawawezesha wateja wa NMB kupata unafuu wa kujikimu kimaisha wakati huo huo wakiendelea na shughuli mbali mbali za kila siku.

Mkuu wa Kitengo cha wajasiriamali Wadogo Wadogo na wa kati wa NMB, Filbert Mponzi (pili kulia) akimpongeza Meneja Mauzo wa kampuni ya Fair Deal Auto LTD, Anil Dewan baada ya kuzindua mkopo wa pikipiki za miguu mitatu kwa ajili ya wateja wa NMB, wakishuhudia ni Meneja Masoko wa kampuni ya Car and General, Jonathani Masanja (pili kushoto) na Meneja wa NMB tawi la Mbezi, Leonard Ngaya.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa kitengo cha Wajasiriamali Wadogo na wa kati, Filbert Mponzi alisema, “Mikopo hii yenye masharti nafuu kabisa, inatolewa kwa mteja yeyote ambaye atatitimiza vigezo vilivyowekwa ili kupata mkopo huu. Mteja mwenye nia ya kupata mkopo huu atatakiwa kuwa na uwezo wa kulipia asilimia thelathini (30%) ya gharama au bei ya Bajaaj au TV’S kama inavyouzwa na wasambazaji wa pikipiki hizi nchini yaani kampuni ya Fair Deal Auto Private Ltd inayosambaza pikipiki za miguu mitatu aina ya Bajaj kwa sasa inauzwa kwa Sh. 5,450,000/= na kampuni ya Car & General Limited Ltd inayosambaza pikipiki za miguu mitatu aina ya TVS King Ltd inauzwa Sh. 5, 600,000/=”.

Mkuu wa Kitengo cha Wajasiriamali Wadogo Wadogo na wa Kati NMB, Filbert Mponzi (kati) Meneja Mauzo wa kampuni ya Fair Deal Auto LTD, Anil Dewan (Kulia) na Meneja Masoko wa kampuni ya Car and General, Jonathani Masanja wakifurahia kuzinduliwa mkopo wa pikipiki za miguu mitatu kwa wateja wa NMB.

Mikopo hii ya Bajaj na TVS King kwa sasa inatolewa katika matawi tisa tu ya NMB yaliyopo jijini Dar es Salaam ambayo ni NMB Temeke, NMB Tegeta, NMB Ilala, NMB Airport, NMB Mlimani City, NMB Mwenge, NMB Mbezi, NMB Magomeni na NMB Msasani. Katika siku za usoni NMB ina mikakati ya kutoa huduma hii katika mikoa mingine ili kuwafikia wateja wengi zaidi.

Mkuu wa Kitengo cha wajasiriamali Wadogo Wadogo na wa kati wa NMB, Filbert Mponzi (pili kulia) akimpongeza Meneja Masoko wa kampuni ya Car and General, Jonathani Masanja (pili kushoto) baada ya kuzindua mkopo wa pikipiki za miguu mitatu kwa ajili ya wateja wa NMB, wakishuhudia ni Meneja Mauzo wa kampuni ya Fair Deal Auto LTD, Anil Dewan na Meneja wa NMB tawi la Mbezi, Leonard Ngaya.

Mkopo huu unaotolewa kwa muda wa miezi 24, ambapo kwa kipindi hiki chote, mteja ataendelea kurejesha makato yake ya kila mwezi kwa taratibu na makubaliano yatakayofanyika baina ya mteja na benki ya NMB. Mikopo hii pia inawekewa bima inayomletea unafuu mkopaji endapo atapata matatizo ya kiafya ambayo yatamfanya asiwe na uwezo wa kufanya shughuli zake za kila siku za kimaisha au kufariki, basi bima hii itachukua jukumu la kumalizia deni la mkopo huu na mteja ataendelea kumiliki pikipiki hii ya miguu mitatu kama kawaida.

Sasa, wateja wa NMB wanaweza kutimiza ndoto zao za kumiliki Bajaj au TVS King kwa kutumia mikopo hii. Benki ya NMB inatoa wito kwa wateja wake kutumia fursa ya kupata mikopo hii kwa unafuu zaidi na kupata fursa ya kumiliki pikipiki hizi za miguu mitatu ili kujikwamua kiuchumi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Bajaj kwa $3500 + 30% interest rate for 24 months. Kweli Tanzania is full of scams and shady deals. Why exploit watu wa hali ya chini? Thats enough money to buy you a ticket to the US na kupiga box na in 24 months turn back home with more money to buy even 25 of those bajaj with cash money to be real

    ReplyDelete
  2. Mdau wa kwanza, huwezi kupata viza ya USA kwa kuwa na 30% ya $3500. Hivi sasa masharti ya viza za ughaibuni ni kuwa uwe na pesa za kuonekana kama huyo bosi hapo katikati. Kuomba viza tu ya ughaibuni basi ni Tsh 1M inakutoka hivi hivi. Na sasa hata ujiripua madole yako wanayo wanakuuliza wewe umekuja na pasi ya TZ kulikoni umekuwa Msomali au Mruwanda sasa?

    ReplyDelete
  3. Trafiki wasiruhusu bajaj ktk miji mikubwa kwani ni kero kwa kusababisha uendeshaji wa vyombo vyamoto barabarani kama bodaboda.

    Hatutaki mfano Dsm central (maeneo ya ndani ya mji) kuzongwa na bodaboda pamoja na bajaj za biashara ya usafirishwaji na kuwa kama Mumbai au Kampala.

    Je, wizara husika, halmashauri ya mji/wilaya na wananchi wameshirikishwa ktk maamuzi kama haya ya kubadili modali ya usafiri mijini central?

    Ni muhimu kushirikisha jamii kupata maoni yao kuhusu mibadiliko ya mifumo ya mji kama usafiri, ujenzi, maeneo ya burudani n.k na siyo kukurupuka kisa kujitengenezea ulaji ambayo utasababisha kero na siyo raha.
    Mdau
    Mkazi wa mjini kati Tanzania

    ReplyDelete
  4. Naungana na Mdau wa tatu 3 anony wa Fri Mar 22, 09:45:00 pm 2013.

    Kwa gharama zote lazima Darisalama yetu iwe ni ya kipekee kabisa.

    Kwa ukwasi tuliopata wa mimali na rasilimali kadhaa tuliyoipata Gas, Oil Uranium and other Madini, hatustahili kutarajia FUTURE kutegemea uasafiri mbovu kama Bajaj na Bodaboda ktk Jiji letu.

    Wakati Mhe. Jakaya Kikwete anaondoka ktk muda wake, tunategemea atafanya juu chini kuziba mapungufu ya Miundo mbinu kama Usafiri wa Mijini na maji Taka yaliyopo ktk miji mikubwa ikiwepo Dar.

    Nadhani tunahesabu siku chache, mitaro ya maji taka itakuwa ni Historia iliyopita, kama tunavyoona Mradi wa DAR RAPID TRANSIT (Mabasi yaendayo Kasi) una kwenda sambamba na uboreshaji wa mifereji na mabomba ya kutiririsha maji taka kwenda kimpangilio na sio helela kama tulivyozoea.

    Hivyo tutegemee vitu kama usafiri wa Bajaj na Bobaboda siku zao zinahesabika kabisa ktk Miji kama Dar Es Salaam!!!

    ReplyDelete
  5. Nakubaliana na wadau namba tatu na nne kwa kweli bajaji katikati ya jiji la Dar es Salaam ni balaa tupu.

    Utaona bajaji imewekesha mlolongo mrefu wa foleni kwenye barabara ya Ali Hassan Mwinyi na madereva inabidi wafuate spidi ya bajaji, hasa ule wakati wa heavy traffik.

    Tumeondoa vipanya kwa nini tunakaribisha bajaji?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...