Mamia ya wananchi wakijiandaa kumlaki Waziri Mkuu wa Denmark Mhe Helle Thorning-Shmidt kupitia lango la Mashariki la Ikulu Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Waziri Mkuu wa Denmark Mhe Helle Thorning-Shmidt Ikulu Dar es salaam leo.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mgeni wake Waziri Mkuu wa Denmark Mhe Helle Thorning-Shmidt wakiingia Ikulu huku wakishangiliwa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika maongezi ya faragha na Waziri Mkuu wa Denmark Mhe Helle Thorning-Shmidt leo Ikulu.
Inasikitisha kuona wazee na watoto wameacha kazi zao na kwenda shule kumshangilia waziri mku wa Denmark. Misaada itakayokuja hapa hawa wananchi na hata wewe Michuzi hutofaidika nayo bali wanakula wao viongozi na familia zao. Ee Mungu we tunusuru sie wanao.
ReplyDeleteAISE MSEMAJI WA KWANZA UMESEMA UKWELI WENYEWE.
ReplyDeleteKILA KIONGOZI AKISHABIKIA KITU SIO KWA FAIDA YA WALE ANAOWAONGOZA LA HASHA. NI KWA FAIDA YAKE NA FAMILIA YAKE
Wadau wa kwanza na wa pili, mmesahau ya kuwa ktk ulaji wa halaiki kwenye masinia mfano ubwabwa inakuwaje?
ReplyDeleteSi kila mlaji anavutia nyama ziwe kwake na kumega tonge kubwa kubwa na kwa haraka?