Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la mchezaji mkongwe wa Yanga na baadaye Kocha wa Pan Africa Marehemu Athumani Kilambo leo Machi 11, 2013 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. Marehemu Kilambo, ambaye alifariki jana usiku baada ya kuugua saratani ya koo kwa takriban miaka miwili, atakumbukwa kama beki imara wa Yanga na Kocha stadi wa Pan Africa ambaye aliiwezesha Klabu hiyo kutwaa ubingwa wa taifa mwaka 1982. Pia amefundisha nyota wengi wa kandanda nchini wakiwemo kina Kassim Manara, Adolf Richard, Mohamed Mkweche, Juma Pondamali na wengineo wengi ambao walichezea Taifa Stars kutokea Yanga na Pan.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiondoka baada ya kuongoza maelfu ya waombolezaji katika mazishi ya mchezaji mkongwe wa Yanga na baadaye Kocha wa Pan Africa Marehemu Athumani Kilambo leo Machi 11, 2013 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa Yanga Lawrence Mwalusako katika mazishi ya mchezaji mkongwe wa Yanga na baadaye Kocha wa Pan Africa Marehemu Athumani Kilambo leo Machi 11, 2013 katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam. wengine toka kushoto ni Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika. Ndugu Adam Malima, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam Mhe Ranmadhani Madabida, Katibu Mkuu wa Pan Africa Saad Mateo na kulia kabisa ni Mwenyekiti wa Yanga Bw. Yusuf Manji. 
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kaka michuzi naona unawakumbuka vizuri wadau wote wa timu kongwe za mjini miaka hiyo.Tena imekua vizuri wote wamekutanishwa na tukio hili, imekua aghalabu kuwaona au kuwasikia wadau hawa wa soka japo wangali hai.
    M/mungu amlaze mahali pema mwenzetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...