Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam leo akiwa ameongozana na mkewe Mama Salma Kikwete kujionea mwenyewe jengo lililoporomoka asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Mkuu wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Bw. Suleiman Kova na Mkuu wa Mkoa huo Mhe saidi Meck Sadiki katika eneo la jengo lililoporomoka mtaa wa Indira Ghandi jijini Dar es salaam asubuhi saa mbili na nusu leo Machi 29, 2013 ambapo hadi Rais anafika mahali hapo saa saba kamili watu wawili wamethibitishwa kuwa wamekufa na wengine 19 kujeruhiwa, wawili wakiwa mahututi. Juhudi zinaendelea kuokoa watu wanaosadikiwa kunaswa kwenye kifusi cha jengo hilo lililokuwa limefikia ghorofa ya 15, likijengwa ubavuni mwa Msikiti wa Shia Ithnaasheri.







Poleni watanzania wenzangu wote.
ReplyDeleteKuna jambo moja huko nyuma niliwahi kulisema lakini michuzi akalitilia kapuni nalo ni la watu kumiminika sehemu ya tukio kiasi cha kwamba hata watowa huduma na waokozi wanakuwa na kazi ngumu ya kufika katika sehemu ya tukio pamoja na kufanya kazi zao.
Picha hizo hapo ni ushahidi mkubwa ni vigumu kujua ni nani ndio in charge na nani hahusiki hapo na ni nani ni kibaka anatafuta chance ya kuiba chochote
Watanzania tuwe na tabia ya kuweka nafasi kwa wahusika kufanya kazi zao katika ajali kubwa kama hizi. Ni vigumu kwa jamaa wa walioathirika au kutojulikana kutofika sehemu ya tukio lakini ni muhimu kutowa ushirikiano na waokozi, madaktaru na askari kwa kuwapa nafasi ya kufanya kazi zao kwa wasaa.
Kila kiumbe kitaonja Mauti inshallah mola awatie moyo wa subrah wale wote waliofiwa na Jamaa zao
ReplyDeletepoleni jamani inasikitisha
ReplyDeleteuzembe huu lazima ufanyiwe kazi na wote waliohusika wakamatwe mara moja
ReplyDeletewww.supermzigo.blogspot.com
Jengo lenyewe mbona michanga mitupu!!
ReplyDeleteHii siyo mara ya kwanza jengo kuporomoka mjini Dar tena maeneo ya Kariakoo! Kuna wakati jengo iliporomoka wlaigunda cement ndo ilikuwa hafifu. Katika Ujenzi hakuna Cost Cutting.
ReplyDeletePoleni sana wafiwa.
Mimi nataka nijue wahandisi hawa walisoma chuo gani, maana nataka nikifunge chuo hicho wasituzalishie wakandarasi uchwala hawa, gholofa zenyewe 5, mnashindwa kudhibiti ubora, je zengekuwa gholfa 50, si vingekuwa vituko, ndo maana watanzania au watu weusi tunadharauliwa siku zote.
ReplyDeleteJanga hili ni aibu kwa taifa letu, wananchi hatutakiwi kuingilia kazi za wachunguzi , wachunguzi watafanya kazi zao. Sisi kama wanachi tunaitolea macho serekali yetu, tokea tukio hili litokee leo ni ya pili , bado kuna waathirika waliolaliwa na kifusi hiko , kweli sisi kama nchi tunashindwa kuokoa majanga ya baharini basi hata haya ya nchi kavu. Kuna watu ambao wamelaliwa na kafisu hiko bado hawajaokolewa Ina maana watu watakufia humo kwa kukosa msaada tu. Je serekali mpaka sasa imefanya hatua gani?
ReplyDelete