Rais msaatfu wa  Finland (2000-2012) Mama Tarja Halonen akiwa shopping jijini Helsinki bila walinzi wala gari. Alipomaliza alipanda treni na kurejea kwake bila kelele wala mikwaruzo...


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 27 mpaka sasa

  1. Maskini ndio tunajua kujitutumua walinzi kibao, magari lukuki lakini wafadhili wetu simpleee....!

    ReplyDelete
  2. sasa kazi iko hapa bongo barabara hatuna magari milioni mia nane na vingora kama mia mbili kwa ajili ya viongozi wastaafu kuanzia marais na waziri wakuu na wengine wana wake wawili wawili hao ma gali frendi ndio usiseme sasa kila saa wako barabarani tuwapishe imekuwa tabu tupu na zogo.
    iko haja ya kutokuwapa ulinzi hawa wastaafu wala vingora na misururu ya magari kwani akitamani ashikirimu au kahawa ya bahalesa basiapelekwe kwa vingora na magari sita kwa kwenda kunywa kahawa ya shilingi mia tano amabayo huenda akanywa bure kwa kuwa anakarimiwa.
    muoneni huyu mama anadunda kwa miguu kama hakuwahi kuishi ikulu acheni ubwanyenye umaskini ni akili sio mfuko.
    asante.
    mdau.
    mbeya.

    ReplyDelete
  3. Hii ni nchi tajiri. Kinatushinda nini sisi Maskini?

    ReplyDelete
  4. Kwa kweli nchi nyingine raha kweli. Mwaka jana hapa Gaborone Botswana nilikumbana na Rais mstaafu Festus Mogae wakati nachukuwa mzigo wangu baada ya kutelemka kutoka kwenye ndege ambayo na yeye alikuwa amepanda. Mzigo wangu ulifanana na wake kwa hiyo akakosea akataka kuchukuwa wa kwangu. Nikamwambia kuwa anachukuwa mzigo wangu. Baada ya kuangalia vizuri, akagundua kuwa ule mzigo siyo wake. Akaniomba msamaha, akachukuwa mzigo wake na wote tukaondoka. Muda wote huo mimi sikujua kuwa ni Mogae. Mwenzangu niliyekuwa nimesafiri naye mbaye ni mwenyeji wa Botswana (Mtswana) ndiye akaniambia kuwa nikiyekuwa naongea naye ni Rais mstaafu wa Botswana. Sikuamini kwa jinsi alivyokuwa simple, bila ulinzi. Na kwa unyenyekevu wa kuniomba msamaha. Kwa hiyo hilo linawezekana Africa pia.

    ReplyDelete
  5. Hakuiba akiwa madarakani. Hakutenda hovyo. Hana cha kuogopa.

    ReplyDelete
  6. kwa sababu viongozi watu wanajipachika ukubwa kwa hila , hivyo huogopa kutembea peke yako ili wasipate joto ya ....... kama wangechaguliwa kwa uadilifu na imani wasingekuwa na haja ya kulindwa , tena wakipita na magari yao spidi mtu utafikiri wamebeba mgonjwa mahututi anapelekwa muhimbili

    ReplyDelete
  7. Bongo mtu akiwa kiongozi anataka hata kuku wake bandani watambuliwe kua ni wa kiongozi!

    ReplyDelete
  8. Sisi! Maskini hakipata ....

    ReplyDelete
  9. Huyu Rais Mstaafu Mama wa Finland alikuwa Rais miaka 12 Ikulu.

    Mama huyu na ma-Rais wa aina yake wanaamini miundo mbinu iwe vibaraza vya kutembea kwa miguu kwa ajili ya shopping, mfuko wa rambo alioshika, treni n.k vyote ni kwa ajili ya wa-Finnish wote.

    Lakini huku kwetu mfano TZ na Afrika vibaraza vya kutembelea vinaachwa kuwa na mashimo, treni zinaachwa kuwa chakavu, usafiri wa fujo wa daladala, huduma za afya, shule, elimu n.k kwa vile miundo-mbinu hiyo si ya viongozi kutumia!

    ReplyDelete
  10. muwe mnajaribu kutofautisha viongozi wa huko nyumbani au africa kwa jumla ni viongozi ambao sio waadirifu

    kiongozi inawezekana kabisa ikawa raia hawamtaki na akatumia njia mbali mbali kuendelea kuwa madarakani matokeo yake hujijengea uadui kila kona ya nchi

    hawa viongozi wa nchi zilizoendelea huwa wanafanya kazi zao kwa kukubalika na raia wake ikiwa kuna tatizo ambalo raia hawamtaki kiongozi wao hutumia uwezo wao wa kisheria kumtoa madarakani

    viongozi wa nchi za ulaya hawana wasiwasi wala uwoga kwa raia wao maana hakuna baya wanalowatendea kwa maana kama kuna baya basi raia wana uwezo wa kuwatoa madarakani

    hapa uholanzi viongozi mbali mbali wa juu huwa tunakutana kwenye supermarket au madukani bila kuwa na ulinzi na wengi wao hutumia baskeli kuwafikisha safari zao za hapa na pale

    sasa msitegemee kuwa viongozi wetu wa huko nyumbani watakuwa karibu sana na raia kiasi kwamba wajiamini watajiamini vp na ikiwa hawaaminiwi?

    ni safari ndefu mpaka tuwafikie wenzetu.

    ReplyDelete
  11. Sijui itakuwa lini huku kwetu bongo!!Maana kiongozi bado anavaa mnasimamishwa barabarani kumsubiri apite. Aibu na iwe kwao.

    ReplyDelete
  12. Hapa kwetu kuna watoboaji wa macho. Rais mstaafu akitembea namna hii watamuwekea dawa zile la liquid form, au vidonge; watamchunguza kwa kutumia mabibi wale wa barabarani; watamteka nyara kumpeleka asipopajua kama vile kigamboni, wakamtoboa macho na kumnyofoa kucha, na kummwagia tindikali; na kumfanyia kitu mbaya kama ile ya morogoro au ya Igunga.

    ReplyDelete
  13. Inabidi viongozi wabadilike jamani wanajikweza sana!

    ReplyDelete
  14. Kila nchi ina tamaduni zake. Je mbona hamjiulizi kwanini Marais Wastaafu wa Marekani au Mawaziri Wakuu Wastaafu wa UK hawafanyi hivyo? Sheikh anafanya mazoezi tu kamwagiwa tindikali.

    ReplyDelete
  15. Mnapiga kelele za nini mbona waziri mkuu mstaafu mzee Warioba anadunda mwenyewe?!

    ReplyDelete
  16. WATANZANIA TUNASIFA DUNIANI YA KUWA MADOMO KAYA TU (how to get nothing from everything). MANENO MENGII LAWAMA NYINGI NA HATUCHUKUI HATUA. WEWE UNAEPIGA DOMO HUCHUKUI HATUA, WENZAKO PIA HACHUKUI HATUA, MIMI PIA SICHUKUI HATUA, VIJANA NA MAOFISA BINAFSI HATUPIGI KURA, KUKEMEA MAOVU HATUWEZI BALI TUMEJIUNGA, KUHAMASISHE WENZAKO WACHUKUE HATUA MADHUBUTI HUTUWEZI, BASI TUNATAKA MAMBO YANYOOKE YENYEWE. HAWA VIONGOZI WETU TUMEWAWEKA WENYEWE MADARAKANI MIMI NA WEWE NA BABAKO, MAMAKO NA NDUGU ZAKO, HIVYO KILICHOBAKI NI HESHIMA KWAO. ALEXBURA DAR

    ReplyDelete
  17. Hapa mkiwa wakurugenzi mnataka magari ya fahari na mkipita katika corridors mnapiga miruzi ya nyimbo za kwaya. Tena wanakuuliza wewe unapata daladala utaibiwa. Na watoto vilevile wanawaambia wenzao shuleni sisi baba etu hataki tupande daladala. Siku si mnaona kila mtu ana gari tena anasema nimejikomboa siijui daladala siku hizi. badala yake ndio anasababisha misururu barabarani kwa starehe za mbwa kukalia mkia. Watanzania ni washamba toka viongozi, wakurugenzi, mamanager, na hata makarani wana attitude fulani hivi, sijui kama itabadilika hata serikali ikibadili magwanda, hicho kitu kiko katka bongo zao.

    ReplyDelete
  18. Aliongoza nchi yake vizuri kwa heshima na adabu, kwa nini augope kutembea mitaani?

    ReplyDelete
  19. Viongozi wa Marekani na Uingereza hawako huru kwasababu wameua watu wengi Iraq, Afghanistan, Kosovo, you name it. Mzee Warioba yuko huru kwasababu hajaiba!

    ReplyDelete
  20. Utajiri ama kuimarika Kiuchumi hakuji bila kubana matumizi.

    Hakuna njia ya muujiza kupata mwamko wa Kimaendeleo bila ya kupunguza matumizi na maisha ya juu.

    Hao ndio Wahisani wetu wanaotoa Misaada kwetu wao Viongozi wao Wastaafu wanapanda Matreni na wanaenda kwa Miguu.

    ReplyDelete
  21. Hii ni dalili ya mtu muadilifu, huyu hakuuwa mtu wala kudhulumu mtu katika utawala wake, na Mkapa nae afanye hiv.

    ReplyDelete
  22. Viongozi wa Marekani hasa hasa George Bushi hawawezi kutembea bila ulinzi why? na viongozi wengi wa Ulaya kama vile wa Ufaransa na Wiingereza wanatembea na ulinzi mpaka leo why? ni Nchi chache sana ambazo zinamifumo ya usawa kama vile Nordic Countries na Africa Botswana ni mfano.

    ReplyDelete
  23. njooni ZANZIBAR MUANGALIE MAWAZIRI WASTAAFU WANAUZA TUNGULE (NYANYA)SOKONI, MNASHAANGA ULAYA KUFANYA SHOPPING WAO PESA WANAZO BADO. WENZIWAO HUKU BAADA YA KUSTAAFU HAWANA NA KUAMUA KUA WAJASILIAMALI WADOGO

    ReplyDelete
  24. Mtusimshangae sana huyo mama. na hili nalo ni la kushangaza. Pope Francisco I alipoteuliwa tu, na kumaliza pilikapilika za pongezi alirudi mwenyewe hotel aliyoshukia, akalipa bill yake mwenye na kuchukua mizigo yake mwenyewe kurudi vatican kuanza kazi. kumbuka pope ni kiongozi wa DUNIA na siyo wa nchi moja kama walivyo hao wengine. kwa hiyo inawezekana kwa wakuubwa kujishusha, na siyo watu wenye madaraka kujikweza na kujiona iungu watu. hata pope alivyokuwa cadinal alitumia usafiri wa umma na siyo vx kama wengine.

    ReplyDelete
  25. Bongo Tambarale:

    1.Ukitembea kwa miguu ilhali ukiwa wewe ni Bosi, watakuita Unafanya Ushirikina ama ni mashariti ya Mganga wako!

    2.Ukiwa na fedha ama hata kama ni siri yako unazo lakini ukienda kwa miguu unaitwa Masikini!!!

    Bongo heshima ya mtu ni kuwa na gari!

    ReplyDelete
  26. Zamani zile waziri mkuu wa Sweden aliuawa naye alikuwa na tabia kama hii. Nadhani alikuwa anatokea movie, hivyo ni high risk

    ReplyDelete
  27. Mdau hapo juu umenifurahisha sana; nikija likizo nyumbani nikiukanyaga kuepuka foleni wananchi wananishangaa. Yaani nikae kwenye gari foleni ya Baruti mpaka Ubungo kisa nionekane nina pesa, nikitembea naonekana masikini. Hiyo ndio tamaduni ya Watanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...