
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa
jana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo,Alex Msama
ilieleza kuwa msanii huyo amepata asilimia kubwa ya mashabiki wanaotaka
atumbuize kwa waimbaji wa ndani, hivyo tayari kamati yake imempitisha
kushiriki tamasha hilo.
"Tunaendesha kura ya maoni kwa mashabiki
wetu kwa njia ya kutuma ujumbe mfupi wa maandishi au kupiga simu
kuelezea ni waimbaji gani wa ndani ya Tanzania na nje ya Tanzania
wanaotaka wawepo kwenye tamasha la mwaka huu.
"Kwa hiyo mwimbaji
Rose Muhando amepata asilimia kubwa ya mashabiki wanaotaka awepo, zaidi
ya asilimia 90 wanamtaka Muhando.
Hivyo huyo tayari anakuwa tumeshampitisha tunaomba mashabiki waendelee
kutuma maoni yao kwa kamati yangu ili kupitisha wasanii wengine.
"Dhamira
ya tamasha letu mwaka huu ni liwe la aina yake na tuwashirikishe
mashabiki wetu, ndiyo sababu kuanzia mikoa litakapofanyika mpaka suala
la waimbaji tumewapa fursa mashabiki wenyewe wateue," alisema Msama na
kuongeza kuwa msanii atakeyekuwa amepigiwa kura kwa wingi ndiye
watakayemtangaza.
Tamasha la Pasaka limepangwa kufanyika Machi 31
mwaka huu jijini Dar es Salaam na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa
Sokoine Mbeya, wakati Aprili 3 ni Uwanja wa Samora Iringa na Aprili 6
Uwanja wa Jamhuri, Dodoma na siku inayofuata itakuwa Uwanja wa CCM
Kirumba, Mwanza.
Tamasha la mwaka jana baadhi ya waimbaji mahiri
waliokuwepo ni Rose Muhando, Rebecca Malope, Christina Shusho, Upendo
Nkone, Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Atosha Kissava, Ephraim
Sekeleti na kundi la Glorious Celebration.
Pia kwaya
mahiri ya Kinondoni Revival, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zilikuwa miongoni mwa burudani
zilizokuwepo siku hiyo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...