Niwazapo nchi yangu, roho yangu husinyaa

Tokea enzi za tangu, mali za kugaa gaa
Lakini kuna ukungu, mnene ulozagaa
Masikini nchi yangu, wapi tunaelekea?

Tumejaliwa na Mungu, kila chenye manufaa
Watu, ardhi na mbingu, kote vimetapakaa
Bado tuko kwenye pingu, pakutokea hadaa
Masikini nchi yangu, wapi tunaelekea?

Tulianza wanguwangu, uhuru kupigania
Tukawan’goa wazungu, ili tubaki huria
Tukayapita machungu, nchi tukashikilia
Masikini nchi yangu, wapi tunaelekea?

Tukalikamata rungu, dola kuishikilia
Wakatupisha vipungu, nchi wakatuachia
Na ndipo kizunguzungu, kikaanza kutitia
Masikini nchi yangu, wapi tunaelekea?
  
Sera za kinyungunyungu zikaanza kutokea
Tukataifisha vyungu, kupika hatujajua
Uchumi ukawa gungu, ngoma ya kizazaa
Masikini nchi yangu, wapi tunaelekea?
  
Tukaanzisha ukungu, elimu kuihadaa
Tukakiacha kizungu, kama lugha fundishia
Kiswahili kawa dungu, bila ya kukiandaa
Masikini nchi yangu, wapi tunaelekea?
  
Elimu kawa Kurungu, aliyepotea njia
Tukaunda Kiswazungu, lugha ya kupotezea
Elimu mwogo mchungu, usomapo Tanzania
Masikini nchi yangu, wapi tunaelekea?

Na Shafi Kaluta Abedi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. TUNAELEKEA CHOONI MJOMBA.

    ReplyDelete
  2. Bwana mdogo Shaffi hebu nitumie email kwenye anwani yangu ya nkwazigatsha@yahoo.com tuchonge sana baada ya siku nyingi. Kumbe bado unaendeleza fani yetu siyo?

    ReplyDelete
  3. Sasa kama wakati wa kusoma uko kwenye blog ya issa michuzi, facebook, twitter, na mablog yote ya tanzania uende katika matamasha ya kila leo ya bure na ya kulipa cocoa beach, nyumbani, kule zakhem sijui inaitwaje halafu uweze kujui formla za hesabu zote, na physics na chemistry na mwanamutapa, na siasa za mwalimu nyerere. Hebu iangalie hio concoction hiyo haba ambayo hata sijaimalizia kweli kitabu kitapanda. Hata hao waseminari ambao wamesoma sana actually wamepasi mitihani, lakini elimu hawana.

    ReplyDelete
  4. wakipewa homework wanapeleka mwalimu wa twishen afanye.

    mbona siku ya mtihani hamkumpelekea asovu?

    ReplyDelete
  5. Wewe Mwandishi ndio unatakiwa ushiriki kuiokoa nchi badala ya kusihia kuandia Mistari tu.

    Ingia kwenye Chama tena Chama cha Mapinduzi halafu lete changamoto zako kuleta mabadiliko ukiwa ndani ya Chama!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...