Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akitoa Tamko kwa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu Siku ya Afya ya Figo Duniani itakayoadhimishwa tarehe 14, Machi. Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Figo Tanzania ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali Frederick Werema.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Figo Tanzania Mh. Frederick Werema akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu umuhimu wa kunywa maji safi na salama kama moja ya njia za kukinga figo kuathiriwa na magonjwa mbalimbali na kutoa wito kwa watanzania kuepuka tabia hatarishi kwa afya ya figo zikiwemo za utumiaji wa pombe kupita kiasi, madawa ya kulevya, utumiaji wa dawa za binadamu kupita kiasi na uvutaji wa sigara. 
Katibu wa Taasisi ya Figo Tanzania Dr. Linda Ezekiel akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu mikakati ya Taasisi ya Figo Tanzania katika kutoa kwa elimu wananchi na mchango wake katika kupambana na ugonjwa wa Figo nchini.
 Picha na Aron - MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...