Ni vyema wananchi wote wakafahamu kuwa ni kosa kwa mtu au taasisi yeyote ile kuchukua Matangazo ya Sekretarieti ya Ajira na kuyafanyia marekebisho au kuandaa matangazo mbalimbali yanayohusiana na mchakato wa ajira katika Utumishi wa Umma kwa lengo la kupotosha umma ilihali wakijua wazi kuwa taarifa hizo wanazozichapisha au wanazoziandika katika mitandao ya kijamii hazijatolewa na Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.
Tumefikia hatua ya kusema haya kutokana na baadhi ya taarifa zinazohusu mchakato wa ajira hususani uwepo wa nafasi za kazi zilizopo katika baadhi ya mitandao ya kijamii ikionyesha kuwa Katibu wa Sekretarieti ya Ajira ametoa matangazo hayo.
Moja ya tangazo hilo la kughushi na lenye nia ya kupotosha umma ni lile lililoko katika anwani hii www.eastafricajobscareer.com lenye kichwa cha habari kinachosomeka “Tangazo la Kazi Utumishi Tanzania June 2013”ambalo linaonyesha “Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 8 Juni, 2013”.
Hii websie ina matatizo ya kiufundi na si kwa tangazo lenu tu. Ni kwamba matangazo ya mwaka jana (2012) yanaonekana ni ya 2013. Hii si kwa tangazo lenu tu kwa mfano kuna mengine ya Uganda, Kenya, nk yanayosomeka mwisho wa kutuma maombi ni December 2013!Si kwamba taarifa yenu tu ndio imelengwa kwa kugushiwa
ReplyDeletewe ndo mjinga kweli, umeelewa sekretariati walichokosema au hujaelewa?. Tatizo la kiufundi unalijua wewe, lakin likiandikwa tofauti na original ilivyo ndo upotoshaji wenyewe. Na wao hawamuongelei mtu wao wanaongelea tangazo lao na hiyo web imetolewa kama mfano tu. Lakin ww kama mfano wa watu wenye uelewa mdogo sababu unayotoa au kueleza haina mashiko hata kidogo.
ReplyDelete