Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL
unawatangazia abiria wote na wananchi kwa jumla kuwa treni kutoka Dar es Salaam kwenda Mwanza , KIgoma na Mpanda katika
siku za Jumanne na Ijumaa utabadilika kutoka saa 8:30 mchana na kuwa
saa 3:00 usiku kuanzia Aprili 02, 2013.
Aidha na kwa treni kutoka Mwanza kuja Tabora itaondoka saa 1:30 usiku
na ile ya Kigoma kurudi Tabora itaondoka 3:00 usiku. Mabadiliko
haya yanatokana na kuanza zoezi la utandikaji wa reli mpya kati
ya Stesheni za Kitaraka (Singida) na Malongwe (Tabora)umbali wa kilomita
89, kazi ambayo itarajiwa kufanyika kwa saa 8 kila siku na hatimaye
kukamilika baada ya miezi 6.
Uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya
Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Kipallo Aman Kisamfu.
TRL Makao Makuu,
Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...