Fatma Gharib Bilar,Katibu Mkuu wa Wizara ya Ustawi wa Jamii, Maendeleo, Vijana, Wanawake na Watoto- Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akitoa mada wakati wa mkutano wa pembezoni ( side- Event) ulioandaliwa na wajumbe wa Tanzania Visiwani wanaohudhuria Mkutano wa 57 wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa kuhusu Hali ya Wanawake, katika mkutano huo ujumbe huo wa Zanzibar ulielezea uzoefu wake, mafanikio na changamoto mbalimbali katika kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia Visiwani humo. Pamoja na mambo mengine, Katibu Mkuu alisisitiza umuhimu wa ushiriki wa makundi mbalimbali ya kijamii wakiwamo viongozi wa serikali, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Wabunge, vyama vya hiari, wananchi wa kawaida waume kwa wake na zaidi Viongozi wa Madhehebu yote ya Dini ili kufanikisha vita hivyo dhidi ya unyanyasaji wa wanawake na watoto. Kushoto kwake ni Bi Fatma Omar naye kutoka Zanzibar na kulia ni Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi.
Bi. Mira Ihalainen, Mratibu wa Mipango kutoka Taasisi ya Umoja wa Mataifa, UN- WOMEN ambaye alikuwa mmoja wa wazungumzaji wakuu, katika mazungumzo yake, Bi Mira alieleza pamoja na mambo mengine kwamba UN- WOMEN itaendelea kufanya kazi kwa karibu na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Muungano ikiwa ni pamoja na kutoa misaada mbalimbali ya kiufundi na kitaalam katika shughuli zote zinazolenga kumkomboa mwanamke na mtoto wa kike. kulia kwake ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto ( Tanzania Bara), Bi. Kijakazi Mtengwa akifuatilia majadiliano hayo na kushoto kwa Mira ni Afisa Ubalozi, Modest Mero aliyekuwa mratibu wa wa majadiliano.
mjumbe akiuliza swali.

Sehemu ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo wa pembezoni ulioandaliwa na ujumbe wa Tanzania Visiwani.
washiriki wakifuatilia mkutano.

Katibu Mkuu akiendelea kujibu mswali kutoka kwa washiriki waliokuwa bado na hamu ya kujifunza kutokana na uzofu wa Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...