Siku ya Jumanne, tarehe 19 machi, majira ya saa tatu na nusu asubuhi, Baba Mtakatifu Francis, amezindua rasmi utume na utawala wake kwa Ibada ya Misa, katika Uwanja wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, mjini Vatican. kwenye Ibada hii ya uzinduzi Baba Mtakatifu ameongoza Ibada pamoja na Makardinali na Maaskofu wapatao 180 na kuhudhuriwa na Wakuu wa nchi 31, Viongozi wa Kifalme 6, Wana Wafalme 3, Mawaziri Wakuu 11. Ibada hii iliudhuliwa na umati wa watu, sio tu waumini wa Kikatoriki bali hata waumini wa madhehebu mbalimbali na zaidi watu tokea dini mbalimbali. Umati wa watu unakadiriwa kutokupungua 200.000. 

Katika Ibada hii, Baba Mtakatifu alivalishwa Pete ya Petro na Kardinali Angelo Sodano , ikiwa kama ishara ya wadhifa wake. 
Bendera ya Tanzania ilipeperushwa vizuri sana na umati mkubwa wa Watanzania walioudhulia Tukio ili la Kihistoria.

Kwa picha na video ya Tukio ili la Kihistoria mnakaribishwa kutembelea blog ya Jumuiya ya Watanzania Rome:www.watanzania-roma.blogspot.com

Picha zote zimeletwa kwenu na ndugu: Andrew Chole Mhella.

  
                                Baba Mtakatifu akipita kubariki watu 


              Bendera ya Tanzania ikipeperushwa mbele ya Baba Mtakatifu.


                                    endera yetu ikipepea katikati ya Umati wa Watu.

       Kulia ni katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma Ndugu 
Andrew Chole Mhella pamoja na Ndugu Safari Mwacha wakiipeperusha 
                                 bendera ya Tanzania.

              Masista na ma Padri wa Kitanzania wakiifurahia bendera yetu. 
                    Kwa pembeni ni baadhi ya Watalii wa kiargentina.
     Furaha ziliwajaa baadhi ya Watanzania waliokuwepo mbele ya Kanisa 
                                           Takatifu la Mtakatifu Petro.


Katibu wa Jumuiya ya Watanzania Roma ndugu Andrew Mhella Pamoja na Ndugu Safari Silvanus Mwacha na ndugu Dusten wakipata picha ya Pamoja na askali waliokuwepo kwenye kuhakikisha shughuli nzima inaenda salama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Katiba yetu inasema, Serikali haina dini.

    Sasa ni vipi nchi iwakilishwe tena na Dhehebu moja tu, tena kwa Bendera ya nchi ambayo ina watu wa Imani tofauti huku wengine hata dini wakiwa hawana?

    ReplyDelete
  2. jamani nimefurahi sana hadi machozi yananitoka. kilichonifurahisha zaidi ni kule kusikia waumini wa madhehebu mbalimbali walihudhuria na kupata baraka ya pope. hii inaonekana kwamba inawezekana watu kushiriki pamoja katika kuabudu bila shida. na inaonekana kabisa hata haya mambo ya kuuwana kaw ajili ya dini yakatoweka na silaa zikawekwa chini na kushirikiana kwa pamoja. hii ni ishara nzuri kuishi kwa upendo na amanibila kubaguana. tuzidi kumwomba Mwenyezi Mungu umoja huo udumu daima Asanteni.

    ReplyDelete
  3. Safiiiiii.....proud of my country na bendera yetu..... Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  4. kaka jamani pongezi zangu aziwaendee hawa ndugu zetu waliotuwakilisha vyema kwenye ibada ya Pope Francis. Maana bendera haikuwa inabebwa au kupeperushwa ilikuwa inaimbizwa vyema kila Pope alipokuwa anakwenda. Mzidi kubarikiwa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...