Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania(TRL), Mhandisi Aman Kisamfu akitoa maelezo ya namna mvua zilivyoletaa uharibu katika eneo la tabata Mwananchi kwa Wajumbe wa baraza la wafanyakazi wa Wizara ya Uchukuzi leo mchana.Wajumbe wa Baraza hilo walitembelea eneo hilo na kuona uharibifu mkuwa uliofanywa na mvua zilizonyesha hivi karibuni.Kulia kwa Mkurugenzi Mkuu wa TRL ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi,Mhandisi Omar Chambo(Mwenye Shati jeupe).
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Miliki ya Rasilimali za Reli(RAHCO), Mhandisi Benhadard Tito(aliyevaa miwani) akitoa maelezo ya namna RAHCO ilivyojipanga kuboresha njia za reli katika eneo lilioathirika na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha kwa wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wa Wizara ya Uchukuzi leo mchana walipotembelea eneo hilo kujionea namna mvua zilivyoathiri Njia za Reli ya USafiri wa Treni Dar es Salaam.
eneo lililoharibiwa na mvua zilizonyesha hivi karibuni na kuondoa kingo zilizo karibu na Reli katika eneo ya tabata Mwananchi. Wajumbe wa baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Uchukuzi wametembelea eneo hilo leo mchana kuona uharibifu uliofanywa na Mvua hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mhandisi Omar Chambo, akitoa maelekezo kwa Mkurgenzi Mkuu wa Shirika la reli Tanzania(TRL) na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Miliki ya Rasilimali za Reli(RAHCO), wakati wa Ziara iliyofanywa na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Uchukuzi katika eneo la Reli lililoharibiwa na mvua leo mchana.
Uharibifu uliofanywa na mvua zilizonyesha hivi karibuni na kuondoa kingo zilizo karibu na Reli katika eneo ya tabata Mwananchi. Wajumbe wa baraza la Wafanyakazi la Wizara ya Uchukuzi wametembelea eneo hilo leo mchana kuona uharibifu uliofanywa na Mvua hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. haha bongo kweli wanapenda kula yani tukio kama hilo ilitakiwa mhusika mkuu mmoja afike kuhakikisha na kufanyiwa marekebisho

    lakini kwa watanzania hapo kuna tume nzima ambayo imepanga kuacha ofisi zao za uwajibikaji na kufanya ziara maalumu ya kutembelea hilo eneo

    safari kama hizo za kundi zima huwa zina gharama sana maana watatoka hapo wapitie kwenye kula kunywa na badae wagawe hela kwa kila alieshiriki kama posho ya siku hiyo

    kwa mpango huo tanzania tutaendelea kulea ufisadi na ufisadi huanzia kwenye mbegu na hizo mbegu ndio hufika mpaka ngazi za juu

    tutamalizana sana na maendeleo yatachukua muda sana japokuwa tunajisifu kuwa nchi inaendelea

    maendeleo tunayopiga sisi ni maendeleo ya kupigwa kwa muda wa mwaka mmoja kwetu tunayafikia kwa miaka 10
    na yale ya miaka 10 tutayafikia kwa miaka 100

    mungu wabariki wanyonge wa tanzania na wakandamize mafisadi WASHINDWE.

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli hata mimi imebidi nicheke....duh kweli hii bongo land, ndo wataalam wetu hao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...