Na Johary Kachwamba na Eleuteri Mangi _MAELEZO-Dar es salaam
WANACHUO Shule za biashara kutoka vyuo vikuu nane (8) mbalimbali vya Afrika Mashariki wanatarajia kukutana ili kujadili fursa za ajira katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Kauli hiyo ilitolewa jana (leo) jijini Dar es salaam na Rais wa Wanachuo wanasoma masomo ya Biashara (Dar es salaam University Finance Association -DUFA) Maximillian Msuya wakati wanaongea na waandishi wa habari.
Alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kuzungumzia maswala ya sekta ya mafuta na gesi na vilevile watazungumzia mitaala ya elimu katika eneo la Afrika mashariki.
Msuya aliongeza kuwa mkutano huo utaangalia namna gani nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinaandaa wataalamu katika soko la ushindani la ajira za kuajiriwa na zile kujiajiri wenyewe.
Mkutano huo unatarajiwa kufanyika siku ya Jumamosi ya tarehe 16 mwezi huu, katika Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam.
Rais huyo ametaja vyuo vitakavyoshiriki kuwa ni Chuo Kikuu cha Nairobi (UON), Chuo Kikuu cha Kisii na United States International University (USIU) kutoka Kenya.
Vingine ni Chuo Kikuu Ndejje kutoka Uganda na kwa upande wa Tanzania kutakuwa na Chuo Kikuu cha Mzumbe, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo Kikuu cha Ardhi, Chuo Kikuu cha Dodoma, Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na wenyeji Chuo Kikuu cha Dar-es-salaam.
Mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Stegomena Tax.
Nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) kuandaa Wataalamu ili kuajiriwa na kujiajiri:
ReplyDeleteLa muhimu ni kuelewa ukweli uliopo ya kuwa nchi zetu za EAC,
1.Zina different 'Fiscal Deficity' utofauti ktk mapungufu ya mahitaji ya ajira kwenye uchumi wao.
2.Zielewa ya kuwa Upungufu huo utapunguzwa kwa watu kujiajiri kama Makala iunavyoeleza na sio kutegemea Kuajiriwa.
3.Kuelewa kuwa sababu hizi mbili ndio maana Development Partners kama World Bank ,IMF,UN na wengineo wanasisitiza Private Sector as engine of growth kwa kuwa Takwimu zimeonyesha ukuzaji wa Uchumi umechangiwa zaidi na Private Sector especially SME's.
4.Nchi za EAC ziandae Elimu inayoendana na kasi hiyo hapo ktk No.3 juu.
5.Nchi za EAC zielekeze zaidi Elimu ya Ujasiriamali ili kukuza ufanisi ktk engine of growth yaani SME's na kuacha kuwa na Utamaduni wa kuamini kuwa Kusoma ni Kuvuka Vidato, Mafano unakuta Waajiri wanaegema zaidi kwenye Vyeti na Viwango vya Madarasa ya Usomi badala ya Ujuzi na Uzoefu ambavyo ndio muhimu zaidi...Kama vile shariti la Ajira unakuta kazi hii anatakiwa mwenye Digirii 2, au Phd. kitu ambacho kazi hiyo hiyo anaweza kufanya Mjasiriamali aliyepewa Mafunzo Elekezi kwa kozi fupi.