Na Mwandishi Maalum
Imeelezwa
kwamba ujumbe wa amani unaweza kuenezwa
kwa njia nyepesi na rahisi kama ile ya kuwatumia vijana na watoto kutumia
vipaji vyao kuchora michoro inayobeba ujumbe unaosisitiza umuhimu wa
amani duniani.
Hayo yameelezwa na Tuvako Manongi, Balozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,
wakati wa hafla fupi ya maadhimisho ya miaka mitano ya “Jioni ya
Amani”, ambapo Asasi isiyo ya
kiserikali ijulikanayo kama CITYarts
Pieces for Peace ilionesha kwa wageni
waalikwa michoro mbalimbali iliyochorwa na watoto kutoka nchi 62 zikiwamo za
Afrika.
Madhumuhi ya hafla hiyo ambayo Ubalozi ulikuwa mwenyeji yalilenga katika
kuonesha ni kwa namna gani watoto wanavyoweza kuhuburi na kuienzi amani kupitia sanaa ya uchoraji na kwa njia hiyo pia kukuza vipaji vyao.
CITYarts
Pieces for Peace ambayo makao yake yako
New York, imekuwa ikitembelea nchi mbalimbali, na kuwahamasisha watoto
na vijana kuchora iwe kwenye makaratasi, mabango au hata kuta kwa lengo
moja tu la kueneza ujumbe
wa amani.
Balozi Manongi amewashukuru waandaaji wa hafla hiyo
kwa kubuni wazo hilo jema la
kuwahamasisha watoto kutumia vipaji vyao vya uchoraji kuhubiri
amani hasa kwa kuzingatia kwamba mara nyingi mawazo wanayotoa watoto yanakuwa
hayajachakachuliwa.
Naye
Mkurugenzi wa CITYartsPieces for Peace,
Bi Tsip Ben-Haim pamoja na kuushukuru
Ubalozi wa Tanzania kukubali kuwa mwenyeji wa hafla hiyo,
amesisitiza haja na umuhimu kwa jumuia
ya kimataifa kuienzi amani kwa hali na
mali.
Akasema
kwamba uamuzi wa Asasi yake wa
kuanzisha program hiyo ya kuwashirikisha
watoto kupitia sanaa kueneza ujumbe wa amani, imekuwa na mafanikio
sana na kwamba program hiyo
imesambaa katika nchi nyingi.
Michoro
wanayochora watoto na vijana hukusanywa na kuwekwa katika mabango ambayo
waandaaji wa michoro hiyo husafiri nayo
kila nchi wanayokwenda na kuionesha kwa
watu wengine na kwa namna hiyo kueneza ujumbe wa amani kutoka taifa moja hadi taifa jingine.
watoto hawa Linda, Maria, Stephen na Alex nao walipata fursa ya kutoa ujumbe wao wa amani kwa njia ya michoro, michoro hapa wapo bize kila mmoja akichora ujumbe wake alioubuni mwenyewe.
Na utamduni wetu ulikuwapo, watanzania hawa, Eri Fungo na Amiri Koba hawakuwa nyuma kurindimisha midundo iliyosherehekesha hafala hiyo
Mkurugenzi Mtendaji wa CITYart akielezea madhumuni ya hafla hiyo na kubwa zaidi ushirikishwaji wa watoto katika kueneza ujumbe wa amani
Wageni
Balozi Tuvako Manongi akiwashukuru waandaji wa hafla hiyo pamoja na wageni waliofika, katika mazungumzo yake mafupi, Balozi alisititiza kwamba watoto na ambao mawazo yao hayajachakachuliwa.
Wageni waalikwa wakisoma ujumbe wa amani
Wageni waalikwa wakipata kitu kidogo walichangamkia sana Maandazi
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...