Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa,Addo Mapunda akisisitiza jambo wakati hafla fupi ya kuwakaribisha walimu wapya watakaofundisha katika shule zilizopo kwenye Halmashauri hiyo ya Kilwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa,Mh. Abdallah Ulega akitoa nasaha
zake kwa walimu waliofika Wilayani hapo.
Walimu wapya wa shule za msingi na Sekondari ambao
wameripoti na kupokelewa Wilayani Kilwa.
Na Abdulaziz Video,Lindi.
HALMASHAURI ya wilaya ya Kilwa imekabidhi meza nne za maabara
inayotembea kwa ajili ya mafunzo ya vitendo katika masomo ya
Baiolojia, Kemia , Kilimo na Fizikia kwa shule nne za sekondari ikiwa
ni sehemu ya hatua za kukabili changamoto za matokeo mabaya ya shule
za sekondari za wilaya hiyo Hususan katika masomo ya sayansi.
Meza hizo zenye thamani ya shilingi Milioni 24 ikiwa ni awamu ya
kwanza ili ya kuziwezesha shule za zote za sekondari kuwa na Maabara
zinazohamishika.
Tukio hilo lilioenda sambamba na kupokea walimu wapya wa shule za
msingi na Sekondari waliopangwa katika Halmashauri hiyo.
Akiongea katika katika hafla hiyo,Mkuu wa Wilaya ya Kilwa,Abdallah
Ulega sambamba na kuwashukuru walimu hao kwa kufika wilayani humo Pia
alitoa wito kwa Jamii kujenga Nyumba Bora hususan Vijijini ili
kusaidia watumishi wanaopangwa huko kwa huduma za jamii zikiwemo Elimu
na Afya.
kutokana na mazingira ya kusomea kutokuwa yenye mvuto ikiwa ni pamoja
na kukosekana kwa zana muhimu na maabara, na kwamba hatua ya
kusambazwa kwa teknolojia hiyo rahisi licha ya kuwawezesha wanafunzi
sasa kujifunza katika hali iliyobora zaidi kwa vitendo,Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa,Bw Addo Mapunda aliwasihi
walimu hao kufanya kazi kwa kuwa Wilaya hiyo inaupungufu mkubwa wa
walimu hususan vijijini.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Bw Ally Mohamed Mtopa
alitoa ahadi ya kununua kitanda na godoro kwa walimu watakaopangwa
katika KATA yake lakini pia aliwageukia walimu hao kuhusiana na suala
la migomo ya walimu ambapo aliwasihi kutojiingiza katika masuala hayo
badala yake aliwaomba walimu hao kufikisha malalamiko yao kwa Madiwani
ambao ndio wenye maamuzi ya Halmashauri hiyo.
Wilaya ya kilwa ilipangiwa jumla ya walimu 104 wa msingi na 78 wa
Sekondari,Kati ya hao 7 hawajaripoti kwa shule za msingi huku
sekondari walimu 23 hawajaripoti licha ya tarehe zilizowekwa na wizara
kumalizika
Mimi ni mdau wa elimu. Nimefurahi viongozi wa kilwa kuwapokea walimu kwa staili hii, inatia moyo. Hongereni
ReplyDeleteNi habari njema kwa maendeleo ya nchi hii,ila tatizo ni pale makzi ya walimu yanapotia simanzi.
ReplyDeleteNilitegemea atoa taarifa za mikakati ya ujenzi wa nyumba bora za walimu na kama zipo aeleze pia.
Hizi sisa za kuhamasisha watu binafsi wajenge majibu yake mtayaona baada walimu wetu kuchoka fedheha ya makazi duni na kuondoka.
Jamani kwa nini fani ya ELIMU imekosa mtetezi?
Bab kubwa Ulega A.Not sure if u have a time to see this michu blog, if so pliz give me a phone number of u're bro Bwajubwaju au Mauridi.Qweman.Papalla
ReplyDelete