Picture
Yanga vs Ruvu Shootings katika Uwanja wa Taifa, Dar leo
Timu ya Yanga leo imeifunga timu ya Ruvu Shooting goli 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya VodaCom uliochezwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Goli hilo lilifungwa na Hamisi Kiiza “Diego” kunako dakika ya 48 ya mchezo na hivyo kuipa Yanga jumla ya pointi 48 katika ligi hiyo.


Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa kwenye kiwanja cha Manungu mkoani Morogoro, timu za Mtibwa Sugar na Coastal Union zimetoshana nguvu kwa kutoka sare ya kufungana 1-1 na hivyo kufikisha pointi 32 kila moja.



Coastal Union walipata goli lao katika dakika kwanza tu ya kipindi kupitia kwa Ibrahim Twaha “Messi”, goli ambalo lilidumu kipindi kizima cha kwanza. Mtibwa Sugar walisawazisha katika kipindi cha pili.



Hadi kufikia sasa, Azam FC inashikilia nafasi ya pili wakati Simba SC ipo katika nafasi ya tatu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...