BAADHI ya watoto wa Micheweni Kisiwani Pemba hujishughulisha na ugongaji wa kokoto jambo ambalo ni hatari kwa maisha na afya zao,pichaniwatoto wakigonga kokoto kama walivyokutwa na mpiga picha Haji Nassor Pemba.

Ingawaje Serikali inapiga vita utumikaji watoto katika kazi za ajira ngumu lakini baadhi ya wananchi na wazee wanaziba masikio kwa kuwafanyisha kazi hizo,pichani baadhi ya watoto wa Uwandani Vitongoji wakibeba matofali yaliyochongwa kwenye mawe na kuhatarisha usalama wao na kuharibu mazingira
Nikweli lakini hawa watoto mazingira yamewalazimisha kufanya kazi hii.Hiyo serikali unayosema inapinga inamkakati gani wa kuwawezesha watoto hawa ili wasifanye kazi ngumu na za hatari namna hii.
ReplyDeleteWatoto wa viongozi wa serikali wanaburuza vitambi na kugawana rasilimali za nchi kama mazao ya shamba la bibi.Mtoto wa rais ni milionea na watoto wa mawaziri(hata wale vilaza) ndio mamanager wa kampuni na wakurugenzi wa idara za serikali.Kama hiyo haitoshi marafiki wa watoto w vigogo na mademu zao pia ni wakuu wa mikoa na wilaya bali wengine ni wabunge wa kuteuliwa.
Sisi watoto wa macomrade tukale wape kama sio kubeba zege na tofali.
naunga mkona mmoja kwa mmoja kauli ya mdau wa mwanzo hapo juu sisi watoto wa macomrade tukale wapi kama si kubeba zege na matofali
ReplyDeletewanyonge daima mungu atatusaidia si mwinginewe bali ni mungu watoto wa matajiri na wakuu wanasaidiana wenyewe kwa wenyewe na kuchukua mali zao umma kama shamba la bibi well said mdau natamani ningekujua au kukuona ningekupa tano mwanagu
tanzania tambarare oyeee ufisadi oyeeee mtu hutaji tena kwenda shule unahitaji kuwa mjanja mjanja wa kuchota mali za umma
Duh!
ReplyDeleteUmesema ukweli kabisa hapo juu - lakini nani atakusikiliza, wabongo bado tumelala usingizini, labda tutaamka century ijayo. Acha vigogo na watoto wao wale nchi utafikiri hakuna kesho.
ReplyDeleteHata ukimka itakuwa tushachelewa maana kasi ni kali sana wanyonge tutatoka kapa. waache wabebe wasipobeba wataiba.
ReplyDeleteAcheni unyama wa kuwatumikisha kazi ngumu watoto!
ReplyDeleteWapelekeni Shule wakasome kwanza na pia kuwapatia uhakika wa chakula na matunzo.
Uzazi na matunzo mema kwa watoto, sio uzazi na utumikishaji vibaya watoto!
ReplyDeleteHakuna njaa wala nini. Hili ni kosa la wazazi kutowajibika na kutowatendea haki watoto hawa.Africans amkeni, viongozi elimisheni na kuchukua hatua ifaayo.
ReplyDelete