Habari yako Mdau Michuzi!
Leo asubuhi katika mchakato wa kwenda mzigoni town, maeneo ya selander bridge, nilikutana na staili mpya iliyo nikosha roho ya kutoka kwa jeshi la polisi (traffic) ama kama wanavyo julikana 'wazee feva' wakitoa uhamasishaji wa usalama barabarani kwa kutumia bajaj na kipaza sauti kwa madereva barabani.
Hii ni safi sana hasa ukizingatia kuwa inasaidia madereva wote kuhamasishwa na kuwa makini muda wote sababu wanaambiwa wasifanye baadhi ya faulo za barabani kama kutanua kwa kipasa sauti.
nilifanikiwa kuwadaka kwa picha na nimeziambatanisha. Warushie wadau katika blog yako waweze kuona juhudi za jeshi letu likifanaya kazi na big up kwa aliyetoa donation ya bajaj hii amabye ni 'DSM ROAD SAFETY COMITEE' kama inavyoonekana nyuma ya bajaj hiyo.
Asante
Mdau Jerry
Daah....hii nimeipenda
ReplyDeletenimependa hii itasaidia kwa madereva wanao harib barara pembeni.
ReplyDeleteWadau wa 1 na wa 2 mimi nakataa!
ReplyDeleteHivi ni sawa Polisi anayekabiliana na Wahalifu mfano Polisi wa Usalama barabarani huwa wanafukuzana na Majambazi na Wahalifu wa aina kwa aina iweje watumie Bajaj na Waheshimiwa Wabunge watumie 4WD Toyota VX V-8 ?