Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ni eneo kubwa la savana na misitu Kaskazini mwa Tanzania ikitapakaa  katika mikoa ya Mara na Arusha.  Eneo lake ni kilomita za mraba 14,763  na kijiografia inaendelea kidogo ndani ya Kenya katika Hifadhi ya Masai Mara. 
Katika hiifadhi ya Serengeti  kuna idadi kuba ya wanyama  pori. Serengeti inajulikana hasa kwa uhamisho wa kila mwaka wa zaidi ya milioni moja ya nyumbu wanaovuka mto Mara. Kuna pia aina nyingi nyingine za wanyama kati yao "watano wakubwa" wanaovuta watalii hasa yaani tembo, simba, chui, twiga , kifaru na nyati. 
Eneo la hifadhi ya Ngorongoro liliwahi kuwa sehemu ya Serengeti hadi kutengwa kama hifadhi ya pekee. Bonde la Olduvai ambako mabaki ya wanadamu wa kale kabisa yalipatikana liko ndani ya Serengeti. Mazingira ya Serengeti ni kanda ya kijiografia iko katika kaskazini-magharibi ya Tanzania na inaenea kwa kusini-magharibi mwa Kenya kati ya latitude 1 na 3 Kusini na longitude 34 na 36 Mashariki. 
Ina eneo la  mraba kilometa 30,000 2. Serengeti ina gura/uhamiaji ya wanyama kwenye ardhi kubwa na ndefu zaidi dunian, na hua ni tukio la nusu mwaka. Uhamiaji huu ni moja ya maajabu kumi ya asili ya ulimwengu. 
Jina Serengeti limechukuliwa kutoka lugha ya Kimasai, yaani "Serengit" kumaanisha "mbuga isiyoisha". Mnamo mwezi wa Oktoba, karibu herbivores (yaani wanyama wanaokula majani badala ya nyama) milioni 2 husafiri kutoka milima ya kaskazini kuelekea nyanda za kusini na kuvuka mto wa Mara katika harakati za mvua. 
Katika mwezi wa Aprili, wanyama hao hurejea kaskazini kwa kupitia magharibi, na kwa mara nyingine tena huvuka Mto wa Mara. Jambo hili kwa mara huitwa "Circular migration" yaani uhamiaji mviringo. Nyumbu takriban 250,000 hufa safarini wakati wa uhamiaji huu. 
Vifo hivyo mara nyingi husababishwa na kuliwa na wanyama wakali ama uchovu. Uhamiaji huu umeonyeshwa katika filamu na programu nyingi za televisheni kote duniani.Kwa mnaopenda utalii wa ndani si vibaya mkapanga kutembelea hifadhi ya Serengeti
Tembo wakiwa Serengeti
Simba wakila pozi
Swala
Hawa hawana mchezo na mtu...
Pundamilia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Swala sio watu kupenda tu ndio waweze kutembelea kama wahusika wanaweza kuwa wabunifu watapata tu wadau wa ndani kuja kutembelea,kwa mfano mwepesi kabisa kama wenzetu wanavyofanya unatakiwa kuwapa unafuhu wa bei kwa watu wazima (wastaafu)watakuwa na pungozo la asilimia kadhaa labda 50 na wanafunzi wa vyuo asilimia hiyo hiyo ili kuwavutia na muda wa punguzo unaweza wakati ni off peak kwa watalii wa nje ili kucover cost za kuwakidhi watalii wa ndani,lakini bila kuweka pungozo la namna hiyo inakuwa ngumu na tunatakiwa kuwa na holiday package(ukilipa mara moja ina cover kila kitu)sio analipia basi,chakula au fees za mbugani inatakiwa unatangaza bei moja ili mtu ajue inakuwa kiasi gani.Ni hayo na nitarejea kuwapa habari hizi za utalii kwa undani zaidi.........

    ReplyDelete
  2. Ttz sio viwango bali vipaumbele vyetu. Wabongo wangapi wanapenda kutalii,kujifunza mambo mapya ? Wachache sana ila futuhi(komedi), ngoma, na kusadikika hapo utakuta nyomi.Inasikitisha tulivyo. Tunahitaji kubadilika kifikra kwanza.

    ReplyDelete
  3. Tatizo jingine ni kujua bei au Gharama eg malazi chakula nk

    ReplyDelete
  4. naomba kujua gharama za utalii wa ndani au kama waweza nisaidia kupata mawasilliano ya moja kwa moja itakuwa pouwa sana sana

    ReplyDelete
  5. wadau naombeni kusaidiwa kujua gharama za utalii wa ndani ktk mbuga ya serengeti.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...