Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
kusoma hotuba ya Rais kwa mwisho wa Mwezi Machi
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Taarifa ya rais ni nzuri sana na inayotia moyo. Sisi wakristo tumefundishwa kusamehe siku zote 'msamehe saba mara sabini kwa siku hiyo ni jumla 490, tunasamehe siku zote. Kumsomea itikafu rais wetu ni upuuzi usio na maana, nasema mtasoma mara millioni lakini rais wetu hatakufa....atashinda kifo. Tunapaswa tuwe na busara kwani hata mabaya yakimkuta rais atachaguliwa mwingine, hivyo mtakuwa hamjatatua tatizo. Mambo mengi aliyoyasema rais ni ya ukweli kabisa na imani watanzania wenzangu mtamwelewa! Suala moja ambalo nitakuwa tofauti na rais ni hili la kuporomoka kwa ghorofa, mheshimiwa rais kuna tatizo kubwa sana kwenye rapid responce, EMS, na shughuli zote zinazohusu uokoaji. Ni muda mrefu sana ulikuwa umepita hadi uokoaji ulipoanza, nina imani wangeokolewa wengi sana kama uokoaji wetu ungekuwa makini.Hebu tufikiri tu kidogo.....jengo liliporomoka saa 2:30 asubuhi, vifaa vya uokoaji vimeanza kazi saa 4:52 asubuhi,...hii ni baada ya masaa mawili na nusu, sasa katika hali kama hii kuna mtu anaweza kupona ambaye amekuwa trapped na vifusi? Ile oksijeni ambaye ingemsaidia hapo kwenye kifusi inakwisha baada ya dakika fulani k.v 45 au zaidi kidogo. TUTAJIFUNZA LINI? Barabara zetu finyu kwanini zisipanuliwe? kuanguka kwa jengo hilo siyo mara ya kwanza kwenye jiji hilo je tulichukua hatua gani baada ya ripoti ya Lowassa na mapendekezo yaliyotolewa? au tulikuwa tunasubiri janga lingine? Hiyo wizara na wakubwa huko wizarani wanaelewa jengo lilipaswa kuwa la ghorofa 9 inakuwaje lijengwe ghorofa 16 na liwe la chini ya kiwango? kwa nini serikali haiwawajibishi wahusika? au wanasubiri wananchi wasahau kama ilivyo siku zote "as nothing has happened?" Mheshimiwa rais serikali yako ina huruma mno na wabadhirifu na wezi (mafisadi) ndiyo maana tupo hapa tulipo, wananchi wasio na kosa wataendelea kufa kwa uzembe wa watu wachache. Mheshimiwa rais ni aibu kila mara nchi yetu kutolewa mara kwa mara kwenye hizi news outlets kama CNN, CBC, ABCNEWS, BBC, REUTERS, AFP, AP nk kwa mambo ya majanga ambayo ni kashfa kwa wasikilizao na watazamaji....kwa nini tusiwe kwenye hivi vyombo vya habari kwa mazuri? Nina imani wewe rais unachukizwa na haya mambo kama ambavyo mtanzania mwingine yule akiwamo mimi ninavyochukizwa kuona nchi yangu ikitajwa kwa mambo yasiyo mazuri.
ReplyDeleteNimesoma hotuba ya rais neno kwa neno na hakika TZ kuna rais makini sana...nilichogundua ni ukosefu wa uelewa,ujinga mzito na exposure unaowakabili watz wengi.
ReplyDeleteYaani sababu za vurugu zote alizoainisha mh rais kwa kweli kwa mtu makini akizisikia atashangaa sana akili za hao walioanzisha hizo vurugu. Wenzetu duniani wanafikiri sayansi ya hali ya juu sisi tunabishana kuhusu nani achinje?sijui mihadhara?hv kweli kuna watu wana muda wa kukaa sijui na kusikiliza mihadhara?nonsense minds!
Mh rais ningekuwa na uwezo ningependa uje kuwa rais wa hapa denmark maana akili&upeo wako ni wa juu sana ukilinganisha na hao watz...nakuonea huruma mh rais labda ungewaleta hao watz kwa awamu waje waone wanachowaza wenzao wa nchi nyingine.
mdau
denmark
Hivi Jeshi letu la Ulinzi (TPDF) lilikuwa wapi? Si majeshi ya Amerika kwa mara tatu hivi yamekuwa yakifundisha wanajeshi wa Afrika Mashariki kukabiliana na majanga kama hayo?
ReplyDeleteHotuba hii inatia moyo sana..sasa hapo ndo utagundua watanzania wamerogwa na mchawi wao keshakufa kudadekii...Rais yuko pouwa but watu wenyewe ndo hivyo...kila kitu rais????WHY...everybody need to play his/her part sio kila kitu rais...
ReplyDeleteNd.Kikwete nafikiri njia moja ya kutatua tatizo la udini ni kuhakikisha uwiano ktk kila nyanja , kwa mfano kila ukianzia chini mpaka juu hakuna uwiano. Angalia ktk shule za sekondari, vyuo za serikali, utaona wakssto wamepewa nafasi zaidi, angalia ktk mawizara yote ya serikali , jeshi lote liwe la polisi au jwtz au magereza au jkt , nenda mahakamani hivyo hivyo , nenda mahospitali ya serikali ukiangalia hali ndio hio. Kwa hio dawa ya tatizo hili lianzie chini kwenda juu ktk kila nafasi ,sio nafasi za juu tu kama inavyoonnyesha sasa hivi ili kuwababaisha waisilamu, jaribu hili kwanza Rais utaona mafanikio, tusisahau kuwa binadamu wote tuna asili ya kutafuta mafao ili tuweze kuishi , kwa hio kuhakikisha uwiano unadumishwa ndio dawa ya tatizo. Waangalie baadhi ya washauri wako unawalipa mamilioni ya fedha kila mwezi lakini watakupeleka mchomo kama hukuwa mwangalifu.Kabla sijasahau ulipochukua uongozi ktk 2005 kitu cha kwanza ulisaini makaratasi kuwaruhusu masisita kwenye kambi moja ya jeshi nimesahau ilipo ili wajenge ktk ardhi ambayo ya jeshi karibu na kambi ya jeshi , huoni hicho ni kielelezo cha upendeleo? ktk kipindi hiki cha pili umesaini kuepo kwa kamisheni ya vyuo , hili ni tatizo vilevile ambalo litaendeleza matatizo niliyoyazungumzia hapo juu. Kila mmoja ni mchunga na tutaulizwa juu ya majukumu tuliyopewa , kila mmoja ataonja umauti , na hatokufa mtu kwa kuombewa dua yoyote ila kwa ahadi yake , kwa hio huna haja ya kuwa na walinzi na maeskot unapokwenda popote kama unaamini hivyo na kumwamini Mola ndie mkuu , waachishe kazi angalao utapata kuokoa mamilioni ya fedha yanayotumika kuwalipa walinzimwili na makachero wasio na kazi zaidi ya kutumia kodi za walalahoi kununuliwa magari ya fahari na majumba. Nimefikisha...
ReplyDeleteHakuna kitu kibaya kama umaskini wa kufiri na kuona mbali. Ujinga unatawala nchi yetu na si vinginevyo
ReplyDeletenakubaliana na mdau wa mwisho ujinga unatawala nchi yetu na si vinginevyo yote long longa tu eti udini sijui hivi na vile, raisi mzima mwenye akili zake anawesa kusema maneno haya,na anasema kwa manufa ya nani anapata nini na anamuogopa nani kaeni mkitafakari watanzania wenzangu kwa makini msije mkapelekwa puta puta ohooo
ReplyDeletena jamaa wa denmark kaniacha hoi nadhani kaelimika kidogo kuka denmark kwa sabbu inaonyesha dhahiri shahiri elimu bado eti raisi awe wa denmark are you seriousl bro or sis
ujinga ndo umetutawala na anayepata daima hataki kumona munginewe anapata ndo wataleta zao ili kutetea riski zao
fikiriyeni kwa makini watanzania wenzangu huko bongo mlipo wanakudanganyeni sana ALLAH LAKIN YUPO PAMOJA NA NYINYI AMIN
Wewe anon wa Mon 01,11:46 pm inaonekana wewe ni mmoja wa wale watu wanaosema vitu wasivyofahamu au kutokuwa na uhakika nacho. Umesema kuna masista wamepewa sehemu ya kujenga katika kambi ya jeshi halafu unasema hujui ilipo...HIVI UNAELEWA UNACHOKISEMA? sasa kama hufahamu huoni unaleta uchonganishi na kumsingizia rais kwa sababu unazozijua mwenyewe? Sijui utaelewa lini? unasema uwiano unazungumzia uwiano wa nini? unaongea uongo usio na faida, unataka shule ziongozwe na watu wasio na ujuzi tu kwa sababu tu ya imani Fulani, ningekuelewa ungeongelea labda kabila Fulani au rangi Fulani, suala la dini halina nafasi katika nchi yoyote, kwanza dini mtu yeyote anaweza akabadili ndiyo maana nasema ukizungumzia rangi au kabila nitakuelewa. Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu uchungu..unaongelea usilolijua la masista kujenga kwenye imagination yako, kitu hicho hakiwezekani. Mbona hujazungumzia chuo cha TANESCO kilichogeuzwa Muslim university, mbona wakristo hawalalamiki, HIVI NINYI WATU HADI LINI MTAKUWA NA MAWAZO MABOVU? MNAFUNDISHWA WAPI HAYO MAMBO YA CHUKI NA UONGO?
ReplyDeleteNi wasaidizi wake ndiyo matatizo makubwa ya nchi
ReplyDeleteMh Kikwete kweli una hekima kama za mfalme suleiman. Bwana Yesu akulinde na kukutunza my president.
ReplyDeletemdau
norway
Ni mawaziri na watendaji kazi aliowateua ndio wanaleta shida, maana hawajali lolote. If we had 4 Mwakyembes, tungekuwa mbali sana. Iko kazi.
ReplyDeletehotuba nzuri inatia moyo ila tatizo raisi anachelewa sana kutoa msimamo wake,mpaka watu wapige sana kelele ndo aseme,sasa haya maneno ungeyasema mapema ,nani angelalamika? au washauri wako mpaka wadese kwanza ndo wapate hints za kuandika?
ReplyDeleteAnkal next time uwe na version ya audio hat video ya hotuba.
ReplyDeleteNilidhani watu wamekoma kuendelea tu kubishana kuhusu udini... bado tu? TAHADHARI: Ni rahisi mno kumtuhumu John au Juma kua ni mdini, lakini ni vigumu kweli kweli kwa mtoa tuhuma hizo kubaini kwamba yeye pia ana tatizo hilo. Haya ya kuuawa kwa mapadri, kumwagiwa tindikali na kulipukiwa "bomu" masheikh, kuchomwa makanisa na kudhalilishwa vitabu - wachilia mbali kanda za kaseti zilizozagaa... mimi yamenichosha... nyie wenzangu mnaobishana sijui hamjachoka? Jamani, kila tunachokiandika mitandaoni kinasomeka na wengi. Mnapojibizana mkae mkijua hamjengi, mnazidi kua sehemu ya kueneza chuki. Au kama mnataka kuelimishana, basi chungeni kauli zenu. Nikisoma maelezo ya baadhi ya watu, mengi naona yamejaa hasira na hisia zaidi. We must change my fellow citizens. Asilimia kubwa ya watanzania (waisamu au wakristo) wanaolaumu viongozi fulani kua ni wadini, ukiwaambia wathibitishe wamebaguiwa vipi... ni hisia. Hakuna hata mmoja atakayetoka mbele na akathibitisha kwamba yeye binafsi amebaguliwa. Kila mtu anakimbilia kulinganisha idadi ya wenye majina ya asili ya kizungu na kiarabu.... Ni makosa makubwa tunafanya
ReplyDeleteHapa tz ni kiwanda cha uzakishaji chuki:
ReplyDelete1. wakiona mtu kapata chuki huanzishwa
2. wakiona mtu anazuia wizi kwa manufaa ya taifa atazalishiwa chuki.
3. akionekana mtu mwenye hekima...tayari chuki nk nk nk.
Sasa wakristo na waislamu chuki ya nini? au kwa sabb huyu ni mtoto wa bi mkubwa na mdogo?
Pendaneni kwa sabb nyote ni wa baba mmoja. ila hapa malezi ndio tatizo kwa sabb kila mtu kalelewa na mama yake.
Rais alisema kitu kizuri sana. Kuna watu wakikaa wana panga choko choko. Na hili ni shetani limeingia tulikatae.
SISI WOTE WATOTO WA NYERERE, AU MSIKITINI AU KANISANI HATA JAMATIN.
ReplyDelete