Habari Ankal,

Natumai umzima na unaendelea na majukumu yako kama kawaida ya kuliendeleza hili libeneke la globu yetu ya jamii.

Sisi ni vijana ambao tumeanzisha maktaba hapa Pangani, Tanga. tuliwahi kuweka post yetu kwenye globu ya jamii na tukapata muitikio mzuri. Baada ya post ile Prof Mbele kutoka Marekani alituchangia vitabu na
Mr. Rodrick Maro kutoka kituo cha msaada wa sheria naye pia ametupatia vitabu.

Bado tunahitaji vitabu zaidi na tunatoa wito kwa Watanzania waliopo ndani ya nchi na nje ya nchi kutuunga mkono katika hili, kwa kuchangia moja kwa moja au kutuunganisha na anayeweza kutuchangia akiwa ni mtu au shirika, taasisi au kampuni.

Leo naileta habari moja ya mafanikio, tumeweza kuanzisha blog yetu ambayo tutakuwa tukipost mambo yetu na kupokea ushauri na mapendekezo mbalimbali kutoka kwa wadau wote watakaounga mkono jitihada zetu.

Tunapatikana katika www.panganiia.blogspot.com

Karibuni wote.

Kamburuta, Ally Said
Mratibu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hongera, mimi napenda kuona vijana tukiwa sehemu ya jawabu la matatizo na changamoto za nchi yetu na siyo kuwa sehemu ya walalamikaji wakati sisi ndio nguvu kazi ya taifa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...