Kampuni ya
Tumbaku ya Alliance One inajiandaa kutoa msaada wa vifaa vya ujenzi na madawati
497 yenye thamani ya shilingi 28,055,000 kwa shule zilizopo Tabora, Kigoma,
Kahama na Ruvuma. Hii inatokana na maombi kutoka kwa jamii ya wakulima wa
tumbaku katika mikoa hiyo.
Kamati ya miradi
ya maendeleo ya Jamii ya Alliance One ilikutana hivi karibuni mjini Morogoro na
kuidhinisha msaada huu ikiwa ni sehemu ya namna Alliance inavyojitolea kuwajibika
kwa jamii. Mradi huu unalenga kusaidia jamii zilizopo ndani ya maeneo ambayo
Alliance One inaendesha shughuli zake. Sera ya kampuni kuwajibika kwa jamii
inalenga kusaidia katika nyanza za elimu, afya na kutunza mazingira.
Msaada ambao
Alliance one inatoa kwa jamii unaenda sambamba na juhudi za serikali katika
kutoa huduma za jamii kwa watu wake.
“Tunawajibika kwa Tanzania na tunashukuru kwa msaada
ambao Serikali imekuwa ikitoa kwa sekta ya tumbaku na tunaamini kwamba tunawajibika
kusaidia kupunguza umaskini kwa kuchangia katika elimu, afya na kuhifadhi
mazingira,” alisema Mr. Mark Mason, Mkurugenzi wa AOTTL na Mwenyekiti
wa CDPC.
Shule ambazo
zitafaidika na msaada huu ni Shule ya Msingi Kalunde iliyopo Tabora (madawati
110), Shule ya Msingi Imalauduki (madawati 70), Shule ya St. Francis iliyopo Tabora
(mifuko 20 ya mbolea), Shule ya Msingi Mulungu iliyopo Kahama (mabati 50 na mbao
120 za kuezekea darasa moja), Shule ya msingi Lugongoni iliyopo Nguruka, Kigoma
(madawati 70), Shule za Msingi Mkongo Gulioni, Mlindimila na Litete zilizopo Songea,
Ruvuma (madawati 30 kila moja) na Shule ya Msingi Geitasamoi liyopo Serengeti, Mara (madawati 157).
Alliance
One Tobacco Tanzania Ltd (AOTTL) yenye makao makuu yake katika Manispaa ya Morogoro,
maeneo ya Kingolwira, ni kampuni tanzu ya Alliance One International (AOI) ya
Marekani yenye makao makuu North Carolina. Ni moja kati ya kampuni tatu
Tanzania zinazonunua tumbaku na inanunua zaidi ya kilo 35 milioni kutoka katika
vyama vya msingi vya ushirika 182 vyenye wanachama wakulima wapatao 39,800
kutoka Tabora, Urambo, Kahama, Manyoni, Iringa, Kasulu, Songea na Mara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...