
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika Kijiji cha Mwaya, Ulanga, Morogoro, Aprili 15, 2013.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipokea kadi ya Chadema kutoka kwa aliyekuwa mwanachama wa chama hicho, Abeid Mloka aliyetangaza kuhamia CCM, wakati Kinana alipohutubia mkutano mkubwa wa hadhara katika kijiji cha Mwaya, Ulanga mkoani Morogoro, Aprili 15, 2013. Mloka alikuwa miongoni mwa vijana watano walioamua kuahamia CCM papo hapo.

Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib, akionyesha kadi za Chadema ambazo vijana waliokuwa wanachama wa chama hicho waliamua kumkabidhi papo hapo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenye mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika Aprili 15, 2013, kwenye Kijiji cha Mwaya, Ulanga mkoani Morogoro.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Pancras Mogela aliyekuwa mwanachama wa Chadema akipoamua kujiunbga na CCM, Kinana alipotembelea tawi la CCM Viwanjani, Ulanga mkoani Morogoro, kukagua uhai wa Chama kwenye tawi hilo, Aprili 15, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi Mbuzi kwa Nahodha wa timu ya Libenenga, Steven Maundu, baada ya timu hiyo kuibuka mshindi kwa kuibugiza timu ya Nkongo mabao 2-0, katika mechi ya fainali ya Kinana CUP, kwenye Uwanja wa Mwaya, Ulanga mkoani Morogoro, Aprili 15, 2013. Pamoja na zawadi hiyo, ameipatia timu hiyo zawadi ya sh. 100,000 kiasi kinacholingana na alichoipa timu iliyofungwa. Kulia ni Nahodha wa timu ya Nkongo, Abdallah Mazengo.

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi kwa Magdalena Mashinga, alimkabidhi kadi za CCM kwa wanachama wapya kwenye tawi la CCM la Mawasiliano, wilayani Ulanga,Aprili 15, 2013, akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa chama mkoani Morogoro. Kushoto ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib na Mwenyekiti wa CCM mkoa hu, Innocent Edward.

Wananchi wakimshangilia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika Aprilki 15, 2013 kwenye Uwanja wa Mwaya, Ulanga mkoani Morogoro.Picha na Bashir Nkoromo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...