Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman Kinana akizungumza na wakazi wa kata ya Chakwale,wilaya ya Gairo mapema leo mchana,alipokuwa akizindua shina jipya la wakereketwa wa chama hicho.katika uzinduzi huo Kinana aliwaasa  na kuwahimiza wakazi wa eneo hilo kuwa na moyo wa kufanya kazi kwa kijitegemea badala ya kusubiri serikali iwafanyie kila kitu ikiwemo na suala la kuwapa ajira.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdurahman Kinana akiwapa kifuta jasho baadhi ya wazee-waasisi wa chama cha CCM,kabla ya kufanyika kwa uzinduzi wa shina jipya la kata yao ya Chakwale,Wilaya ya Gairo mapema leo mchana.Ndugu Kinana na Ujumbe wake wa CCM wako ndani ya Wilaya ya Gairo katika ziara ya kuimarisha chama cha CCM mkoani Morogoro sambamba na kuangalia shughuli mbalimbali za maendeleo.
Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi-CCM,Nape Nnauye akizungumza jambo mbele ya wakazi wa Chakwale mara baada ya shina la kata hiyo kuzinduliwa mapema leo mchana,ndani ya wilaya ya Gairo.
Baadhi ya Wazee waasisi ndani ya CCM-Kata ya Chakwale wakionesha kadi zao za chama cha CCM walizonazo tangu kuanzishwa kwa chama hicho,kwenye shughuli fupi ya kuzindua shina la kata hiyo.
Kijana aliyekuwa Mwanachama wa CHADEMA akiwa ameinyanyua kadi ya chama chake cha awali,na kukabidhiwa kadi ya chama cha CCM,akiwa mmoja wa wanachama wapya waliojiunga na chama hicho cha CCM.
Baadhi ya Vijana wakiwa kwenye ajira ya kujitegemea,kama waonekanavyo pichani wakitumia mashine aina ya Trekta kupukuchua mahindi.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ni mwanaume wa aina gani huna msimamo?

    vyama vinatakiwa kuwa makini na wahamiaji wa vyama si watu wazuri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...