Ndugu Michuzi,
Shirika la ndege la kisiwa cha Samoa, Samoan airline wameanzisha utaratibu wa kulipia nauli ya ndege kulingana na uzito wa mtu na mizigo. Wenyewe wameiita ' Fare weight' system.The lighter the passenger the lighter the fare. Yaani jinsi unavyokuwa na uzito mdogo ndivyo unavyolipa nauli ndogo. Utaratibu huu umeanza kuanzia mwezi november mwaka jana na watu wamependezwa nao, hata wale wenye uzito mkubwa wameona ni sahihi kufanya hivyo, ingawa wanalipa zaidi kuliko watu wenye mzito mdogo.
Watanzania mnaionaje hii kitu tukii copy & paste? Nadhani ni jambo zuri ambalo vile vile linaweza kuchangia watu kuchunga afya zao hasa swala la kuongeza uzito bila mpango.
Mdau Ruger
Ughaibuni

Yeeheee, Wasamoa ni watu walioshiba sana - hakuna mzaha, they are really huge people.
ReplyDeleteitasaidia watu kudhibiti vitambi aiseee naniii!
ReplyDeleteMimba itakuwaje? Italipia tumbo pia
ReplyDeleteJamaa wana hoja ya msingi kwa kuwa ndege ina limitation ya uzito!!
ReplyDeleteSUMATRA katika kupanga nauli za vyombo vya usafiri walitakiwa kufuata huu utaratibu wa kulipa kadri ya uzito wako.
ReplyDeleteHeee,
ReplyDeleteJamaa wakilijua Soko la Tanzania kwa kweli watapa utajiri mkubwa sana!
Ni vile wa Tanzania tuna hulka mbaya ya kupenda kunenepeana na kufuga vitambi.
ohooo wamiliki wa Mabasi na Madaladala wa Bongo wakisikia hii mbona tutakoma?
ReplyDeleteUtakuta wapiga Debe/Mateja na Makondakita wa Mabasi na mizani mlangoni mwa basi ili kuwapima uzito abiria kabla ya kupanda mabasi!
Mdau hapo juu mimba inatakiwa iwe exceptional otherwise wanawake tutasema tunabaguliwa na safari hii patachimbika - wanaume hakutakalika!
ReplyDeleteMdau - mama mwenye watoto wawili
Kwenye Dala ndiyo watoze kwa Usito na ukubwa wa makalio.
ReplyDeleteMdau wa 3 hapo juu,
ReplyDeleteSula la Mimba ninaomba tusilijadili kwa kuwa kila mmoja wetu hapa lazima atakuwa amezaliwa na mama yake kwa njia ya mimba.
Namuunga Mkono Mdau mama wa watoto wawili anony wa Thu Apr 04, 01:12:00 pm 2013
TAFADHALI KWA SUALA LA MIMBA NA MAMA ZETU TUACHE KEBEHI NA DHARAU !
Wewe Mdau wa tatu unaeongela MIMBA akili zako nzuri kweli?
ReplyDeletePana aliyeweza kuiona dunia bila kupitia ndani ya mimba?