SERIKALI     kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema haitabidili kamwe  maamuzi iliyotoa kuhusu Pori Tengefu la Loliondo, mkoani Arusha na kuwataka wanaharakati wanaochochea mgogoro wa ardhi katika eneo
hilo kuacha mara moja.

Tamko hilo la serikali, limekuja muda mfupi baada ya watu mbalimbali kutoa maoni yao kwenye mitandao na vyombo vya habari kwamba uamuzi wa serikali kuhusu pori tengefu si sahihi.

Tamko la serikali lilitangazwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki hivi karibuni kwamba, wameacha  kilomita za mraba 25,000 kwa ajili ya wananchi na serikali imechukua kilomita za mraba 15,00 kwa ajili ya kutunza rasilimali za nchi.

Alifanya hivyo kwa kwa mujibu wa Sheria ya Wanyamapori Namba 5 ya Mwaka 2009, Sehemu ya 16 Vifungu Na. 4, 5 na 6 na kwamba muda mrefu viongozi wa wizara wamekuwa wakikutana na wananchi na viongozi wa mkoa
wa Arusha na Wilaya ya Ngorongoro kujua kero zilizopo ili zitatuliwe na ndio imewezesha serikali kufanya uamuzi alioufanya.

"Ukweli ni kuwa Waziri Kagasheki alifuata sheria alipotoa tamko kuhusu kupunguza eneo la pori tengefu la Loliondo kwa mujibu wa sheria inayompatia waziri mwenye dhamana uwezo wa kupitia upya mapori tengefu
na kufanya marekebisho mbalimbali muhimu kwa manufaa ya wananchi bila kuathiri uhifadhi,"alisema George Matiko, ambaye ni msemaji wa wizara.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari jana, Matiko alisema tamko lilizingatia tafiti mbalimbali ikiwemo utafiti wa  Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori (TAWIRI) na mapendekezo ya tume mbalimbali zilizoundwa kuchunguza mgogoro wa Loliondo ikiwemo ya Waziri Mkuu iliyoundwa mwaka juzi.

Aliongeza kuwa eneo la kilomita za mraba 1,500 litaendelea kumilikiwa na wizara kwa mujibu wa sheria na kwa kutambua kuwa ni sehemu ya mazalia ya wanyamapori, mapito ya wanyamapori na vyanzo vikuu  vya
maji kwa hifadhi mbalimbali ikiwemo Serengeti.

Alisisitiza ardhi iliyobaki baada ya kuondoa eneo la pori tengefu la Loliondo itasimamiwa na vijiji kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya Vijiji Namba 5 ya Mwaka 1999 na wananchi watawezeshwa ili waanzishe Eneo la Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA) katika ardhi hiyo kwa manufaa yao.

"Tanzania inajali uhifadhi lakini pia inajali maslahi ya wananchi, ndiyo maana asilimia 25 ya eneo la nchi hii limehifadhiwa bila kuwepo migogoro. Hakuna migogoro kati ya wananchi na Serikali, kwa kuwa wananchi wanatambua umuhimu wa uhifadhi kwao na kwa vizazi vijavyo. Ndiyo maana wananchi wanachangia kwa kiwango kikubwa katika kufanikisha uhifadhi,"alimaliza Matiko.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Ombi: Sisi wasomaji wa mitandao hii tunafuatilia kwa kina "Matamko",tumegundua kuwa kuna makosa Lugha yanatumika kwa upande wa Wizara ya Maliasili,katika matamko yanayotungikwa humu ni amri au kalipio kali kuhusu kauli ya wizara.
    yaani kauli hiyo inaonekana kuwa ni kama kitisho au tahadhari.
    Kwa upande mwingine wanaotishiwa ni wananchi watoa maoni ambao wana haki ya kidemokrasia katika kutoa maoni kwa kuandika sasa maoni yasibandikwe jina la uchochezi,vinginevyo wizara yenyewe ndio itajikuta inachochea hasira za watoa maoni,hatimaye wavunja sheria nao wakijipenyeza.Jaribuni kutumia lugha za kueleweka sio kutoa tamko tu na kulisisitiza kwa njia za kijeshi baadala ya kuelemisha wananchi.

    ReplyDelete
  2. To be honest kwa mtazamo wangu "THE GOVERNMENT HAS NEVER BEEN FAIR"

    ReplyDelete
  3. Dah! pic inanikumbusha babu wa loliondo

    ReplyDelete
  4. Hongera Serikali kwa uamuzi kusimamia mlichotamka.

    Jamani siyo siri, nadhani ni wakati muafaka kabisa na kuwaeleza WAZIWAZI ndugu zetu hawa wa jamii ya kimasai kutunza MAZINGIRA. Migogoro mingi inaendelea hapa nchi baina ya wafugaji na wakulima, kwa asilimia kubwa wafugaji hao niwa kimasai. Yaani kana kwamba wao kazi yao ni kuharibu mazingira na kuhamia sehemu nyingine. Nadhani si sahihi kuachwa tu kutembea na makundi makubwa ya mifugo kutoka eneo waliloharibu na kuhamia kwenye maeneo ya KIJANI bila kujali mazingira yetu. Nadhani umefika wakati hawa jamaa waelimishwe kisha wapande miti na nyasi kwa ajili ya mifugo yao nasi kuingia popote kama watavyo.

    ReplyDelete
  5. kweli muosha kinywa hapo namuunga mkono,wizara inapotilia mkazo tamko lake kwa kutumia lugha za vitisho,badala kuelemisha wananchi nini umuimu wa pori lile,pia ni faida kwa vizazi vyetu.
    Wizara unapodiriki kusema msilite uchochezi itajikuta inaanzisha zogo la mtaani,baadala ya kuwaelimisha walalamikaji na kuwajulisha wapi ?pa kupeleka malalamiko yao yatambuliwe kisheria.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...