Kutoka kushoto Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. A. Mgimwa, Mkurugenzi Mkuu wa Africa Group (IMF) Bw. Momodou Bamba Saho pamoja na Naibu Katibu Mkuu Dr. S. Likwelile wakifurahia jambo baada ya kikao cha kujadili masuala ya hali ya uchumi wa Tanzania pamoja na gesi.
 Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. A. Mgimwa akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa Africa Group (IMF) Bw. Momodou Bamba Saho mara baada ya kumaliza majadiliano.
 Ujumbe kutoka Tanzania katika kikao cha pamoja na Mwakilishi Mkazi wa World Bank Tanzania, Rwanda, Uganda na Burundi Bw. Philippe Dongier katika majadiliano kabla ya kukutana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Bw…..
Kutoka kushoto ni Mshauri wa Mkurugenzi wa Afica Group One Bw. Wilson Toninga Banda, Mkurugenzi Mkuu wa Africa Group One Bw. Denny H. Kalyalya pamoja na Mkurugenzi Mwandamizi  wa Africa Group One  Bw. Peter Larose wakiwa katika majadiliano na ujumbe wa Tanzania  ukiongozwa na Waziri wa Fedha Mhe. Dkt A. Mgimwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. World Bank na IMF,

    Kwa sisi Tanzania ukiachilia mbali jirani zetu na wakazi wenzetu wa Ulanda wetu,

    Tanzania kupelekea ujio wa mipango hii ya Gas na Uchumi wetu pana mabadiliko ya aina mbili yanahitajika haraka ama matekelezo:

    A:Mfumo wa Uchumi wetu (Economic Policy)
    Tulisha achana na Siasa ya Ujamaa na kujitegemea, lakini cha ajabu kabisa bado pana mabaki mabaki yake ktk Mfumo wa uchumi wetu has ktk masuala ya Kifedha na Uwekezaji wa sisi wananchi ni kuwa,

    1.CAPITAL ACCOUNT ya BOT bado haijafunguliwa, ni vipi Capital (Mitaji) itafflow wakati uwekezaji huo unahitaji mitaji iingine kuhamishika na kutoka?

    2.BONDS and GOVERNMENTS SECURITIES
    Soko la madeni na dhamana haliruhusu wananchi wa kawaida kuhsiriki ama kuwekeza, hivyo Serikali haipati fedha za kuendesha Miradi kama hiyo ya Gas na Miundombinu au vyanzo vya Mitaji vyenye bei nafuu isipokuwa kwa Mikopo ya nje yenye riba Kubwa, wakati Mitaji hiyo inaweza kupatikana humuhumu nchini kutoka kwa wananchi wa kawaida endapo wataruhusiwa kushiriki. (No local sorces of Capital funds)

    3.SOKO LA HISA NCHINI (DSE),
    Halitoi nafasi inavyitakiwa kwa washiriki watu wa kawaida isipokuwa taasisi huku watu wa kawaida washiriki wakihitajika kutumia Mawakala (Brokers Agents) kuwawakilisha, pia kuweka ukomo wa manunuzi ya Hisa usizidi 60% ktk soko kwa ununuzi mmoja.


    B.Mhimili wa Hifadhi ya Jamii (SOVEREIGN POLICY)
    Haiwezsekani kuelekeza manufaa ya rasilimali kwa wananchi kama hakuna vitu kama hivi chini:

    -Sovereign Funds
    -Social Security Protection
    -Sovereign Registration (vitu kama Vitambulisho vya Taifa)

    Hivyo bila kuwa na vitu hivyo ktk makundi hayo mawili hapo juu A na B itakuwa na ndoto kufikia malengo, kama sivyo inaweza kutokea hadithi ya yaliyojiri Angola ktk suala la Mafuta!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...