Askofu wa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Kusini Njombe Isaya Mengele akiwafungisha ndoa Mhe Philip Mangula na Yolanda Kaberege leo. Katika neno lake, Askofu Mengele amekumbusha Maneno ya Mungu na Kuwataka Wanandoa Kuishi Kwa Misingi ya Dini Kama Ilivyoelekezwa Kwenye Vitabu Vya Dini.
Waziri mkuu Mhe. Mizengo Pinda katikati akifuatiwa na Katibu mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na Mku wa Wilaya ya Njombe Mhe Sarah Dumba.
Kushoto ni msemaji wa familia ya mzee Philip Mangula Dr.Lechion Kimilike ambaye ni Mhadhiri wa chuo kikuu huria cha Tanzania Tawi la Njombe[NJOMBE OPEN UNIVERSITY].
Waziri mkuu Mizengo pinda akisalimiana na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa wilaya ya Njombe bwana Lupyana Fute[Jacky's]ambaye ni diwani wa kata ya Njombe mjini leo wakati wa Harusi ya Mzee Philip Mangula.
Hapa ni ndani ya kanisa la KKKT Dayosisi ya kusini Njombe Mjini ambako pingu za maisha kwa mzee wetu Mangula zimefungwa.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana Katika harusi ya mzee Mangula leo Njombe.
Makamu mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Philip Mangula na Mkewe Yolanda Kaberege leo baada ya kufunga pingu za maisha.
Picha na Gabriel Kilamya
Picha na Gabriel Kilamya
hheeee!!bi harusi mmama kabeba ua naye!!!nimechekaje!!!!Nawatakia maisha mema Mungu awaongoze!!!
ReplyDeleteOh dear....how nice! Wish them long life with full of hapiness
ReplyDeletehehehehehe..hongera sana mwalimu kabelege..Nakutakia maisha marefu kataika ndoa yako
ReplyDeleteDuh Jamaa eeh! Ama kweli wanawake wanabalisha muonekano wa mwanamme...Hebu muangalieni Mzee Mangula leo alivyokuwa sopu sopu...Kile Kitimtim cha nywele na ile midefu yote fyekwa amepigwa ile 'clean face' ya nguvu na anaoneka mtanashati kushinda kijana wa miaka 30:-) Maisha ya ujane kwa kweli ni maisha ya kipweke...Hivyo tunakukia kila kheri Mzee wetu katika maisha mapya ya ndoa pamoja na mama yetu mpya.
ReplyDeleteSasa kilichokuchekesha ni nini? Bi harusi kushika ua ni kawaida. Halafu huyu mzee amekaa muda baada ya mkewe kufariki. Kwa kweli ameonyesha heshima kwa marehemu mke wake. Mungu ailinde ndoa yake.
ReplyDeleteWewe mtoa maoni wa kwanza una matatizo ulitaka ashike magazeti au kamba??hii ndiyo shida yetu kubwa wabongo,wivu na roho mbaya.Ndiyo maana hatuendelei,wangekuwa wana uhusiano nawe ungeandika hivyo?hata wakiwa hawakuhusu tunapaswa siku zote kuombeana mema na mafanikio, kama hujafurahishwa basi kaa kimya ujifie mwenyewe na roho mbaya yako.Mimi siwafahamu lakini nafurahia hatua waliyoichukua.
ReplyDeleteJuzi juzi tu kuna dada katangaza kutafutafuta mchumba toka European Zone acha watu watoe maoni ya kumshambulia kwani alikosea nini?Tumetawaliwa na mawazo finyu, sisi kila kitu ni kuponda tu kwa jinsi hiyo kweli tutafika?bado tuna safari ndefu sana.Mtu anatengeneza maisha yake kwa positive direction sisi tunaua tu na wangeamua kubaki single pia mngepata cha kusema,tubadilike wabongo na kuungana mkono kwenye kila lililo zuri.Maendeleo siyo tu kujenga,kununua gari au kuwa na mamilioni, hata kwa issue ndogo lakini muhimu katika maisha ni hatua moja mbele.
Nawatakia maharusi wapya maisha mema ya amani na furaha.Na yule dada aliyetoa tangazo la kutafuta mchumba Mungu ampe mwenza mwema na mwenye upendo wa kweli asivunjwe moyo na watoa maoni wajinga,na kama kuna wengine wenye matashi ya namna hiyo msisite kufanya au kutoa matangazo yenu.Tuko katika dunia ya utandawazi.
Kila la heri kwetu sote.