Pichani kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa KFC-Tanzania,Bwa.Simon Schaffer akizungumza na Wanahabari kutoka vyombo mbalimbali (hawapo pichani),mapema leo jijini Dar,kuhusiana na uzinduzi wa tawi lao lilipopo Mikocheni karibia na shule ya Feza jijini Dar,Tanzania.Bwa.Simon alisema kuwa wazo la kufungua mgahawa huo nchini Tanzania,ni wazo ambalo limechukua muda wa miaka 3 kutimiza,amesema kuwa KFC itahakikisha viambata vinavyotumika kuandaa vyakula vinapatikana kutoka kwa wasambazaji waliokidhi vigezo vya viwango na ubora,aidha alibainisha kuwa Wafanyakazi wa mgahawa huo (ambao kwa asilimia kubwa ni Watanzania),walipata mafundisho ya miezi 6 kwa malengo ya kuboresha uwezo wao katika kuhudumia wateja kwenye sekta ya vyakula.

"Nasubiri sana kwa hamu kuona jinsi Watanzania watakavyo furahia chakula na huduma za KFC,huduma zetu zimeandaliwa kwa kuzingatia jinsi ya kuwapa wateja huduma kwa haraka na ubora,tunafurahia sana kwa kuanza kuhudumia soko la Tanzania na kuleta huduma tofauti na iliyo bora zaidi",alisema Bwa.Simon.KFC ina migahawa zaidi ya 17,000 duniani historia yake ikianzia huko Kentuky nchini Marekani.
Mmoja wa Wafanyakazi wa mgahawa wa KFC,Faraja Kilongole akifafanua  jambo mbele ya Wanahabari (hawapo pichani), namna walivyopata mafunzo jinsi ya kuwahudumia wateja kupitia mgahawa huo,ambao ndio mara ya kwanza kufunguliwa nchini Tanzania.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mgahawa wa KFC,wakishangilia jambo mara baada kuzinduliwa rasmi na kuanza kuwa tayari kuanza kuwahudumia wateja mbalimbali watakaokuwa wakiwasili kwenye mgahawa huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Umeandika yooote lakini haujasema upo wapi. Haya ngoja tuunge tela la macdonaldization

    ReplyDelete
  2. Tumekwisha, madege Ndani ya Bongo

    ReplyDelete
  3. Kentuky Fried Chicken au KFC kuwa muwazi maana umaarufu wake umeenea duniani kote kulikoendelea

    ReplyDelete
  4. KFC Tanzania?!!!Jamani jamani tunakwenda wapi? Hawa wazungu hawa wanatuletea magonjwa ili waendelee kuuza madawa wanayotengeneza huko nje! Sasa KFC ya nini?Mbona tunavyakula vyetu vi´ngi vya asili, kuku wa kienyeji nk. Hivi hao kuku wanaokaa miaka bila kuoza kweli kweli! Nahurumia sana afya za watanzania, wao wamarekani yameishawaletea ma-obesity sasa wanaona tugawane hayo magonjwa na Tz. KFC sio tija bali bali ni kuongeza magonjwa. Sasa tuna malari, TB na ukimwi vinasumbua sana na haya magonjw vyakula yanahamishiwa Tz ila tutajashtuka ambapo tayari itakuwa too late tutakapoanza kuhangaika na matibabu. Wizara ya afya mko wapi? TFNC mko wapi smbso wapo chini ya MOHSW? Hivi kwa nini kabla ya biashara za vyakula kama hizi kuanzishwa wasishirikishe wataalamu wa afya wanaojua mambo ya vyakula? Au nao wamenunuliwa kiaina aina? Kama walihusishwa this is sooooooo sad! Mungu iponye Tanzania na watu wake.

    ReplyDelete
  5. Jamani tunakwenda wapi? KFC ya nini Tz? Jamani mie nilidhani serikali ina mipango ya kufunga Steers, Merry brown, nk sasa ndio kwanza kuongeza matatizo ya afya kwa watanzania! Kizazi cha watoto wetu kitakuwa cha matatizo ya magonjwa sana! Heri wenye elimu ya kuhusiana na hivyo vyakula watachukua tahadhari, sasa watanzania wengi hawajaelimika kabisa kwenye maswala ya afya hivyo wengi watapata matatizo ya afya, ngoja tusubirie. Msululu wa wagonjwa utaongezeka pia. Ya nini yote haya? Ona wazungu wanavyofurahia jamani sio kila kitu tunakikaribisha jamani tafiti zifanyike kabla ya kukaribisha biashara hizo. nchi yenyewe maskini sana na bado wazungu wanatuongezea umaskini mana sasa unachopata kitakuwa directed kwenye matibabu, hospitalini ama kweli akili ni nywele kila mtu ana zake. Training kitu gani mavitu hayo hayafai kwa afya za watanzania!

    ReplyDelete
  6. Habari nzuri, hata hivyo haijakamilika. Tufahamishwe kuwa huo mgahawa uko wapi, mtaa na jengo hapa Dar!!!

    ReplyDelete
  7. Mgahawa upo Dar sehemu gani?Dar kubwa ati!
    What does KFC stand for?

    ReplyDelete
  8. naamini wauzaji wamepimwa afya zao kabla ya kukubaliwa kufanya kazi

    ReplyDelete
  9. Tunajaribu sana kutunisha uwezo wetu wa vipesa mifukoni. Mara unakuja mrija kutoka nje kufyonza hivyo vipesa!

    Wao hawakuendelea kutokana na wawekezaji wa nje. Walizalisha ili wauze nje!

    Amkeni!

    Amerika inapata ushindani mkubwa kutokana na fast food musrooming; ndio maana KFC wanaingilia nchi za nje kama Tanzania sasa!

    Amkeni kwa kutafuta ujanja wa kuzalisha kuku wenu na kuwapika ki-KFC!

    Mzee Kifimbo Kaburini!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 01, 2013

    Mkuu! Asante kwa taarifa nzuri ya makulaji! Ila wamezingatia afya zetu? Maana pale pembeni kuna daraja ambalo lina mauchafu ambayo sijui yanatoka wapi? Na yamesimama hayajatolewa! TFDA waliona hilo kabla hawajatoa kibali?

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 01, 2013

    Vitu vyenye madhara ni vingi ndugu acha roho ya kwanini!! Basi kama ndoo hivyo viwanda vyote vya pombe vifungwe, wauza sigara marufuku n.k!! Sijui nchi utaiendeshaje? Fikiri kwanza kabla hujatoa wazo lako mdau hapo juu.KFC wapo dunia nzima marekani, ulaya, asia kote wanafanya biashara.Acha soko litaongea, we na familia yako msiwaungishe Sio uwashawishi wengine!wakiona hakuna biashara watafunga vilago

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 01, 2013

    kwani nyie wadau mnaolalamikakuhusu kufunguliwa kwa KFC tz kwani kuna mtu amewalazimisha kwenda kununua vyakula hapo, wazungu wameona opportunity ya kutengeneza hela na wameamua kuitumia ipasavyo. opportunuty oriented interpreneurship..

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 01, 2013

    Mdau wa Nne (4) Anony wa Tue Apr 30, 02:46:00 pm 2013

    Wewe ni Mama Ntilie?

    Unafikiri biashara yako itadoda hao KFC wakiingia nchini?

    Biashara huria ndio hiyo wewe utawapata Wateja wa Daraja lako la Gengeni na wenye nazo watakula huko KFC unaogopa nini sasa?

    Kama ni suala tata la Uchinjaji ktk maadnalizi ya vyakula, Mwekezaji KFC atazingatia KANUNI ZA UCHINJAJI nchini Tanzania kama Mzee Mwinyi alivyofafanua na kama Sheria zetu zinavyoeleza!

    Wewe hutaki tupatiwe Viwango vya vyakula vya Kimataifa?

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 01, 2013

    Wadau Kasi hii ni kutokana na Neema za Gas ,Oil and Minerals ambazo tumezikamata.

    Wawekezaji hadi wa kuzoa Vinyesi na Majitaka huvutiwa na sehemu zenye Utajiri wa rasilimali, kwa kuwa hakuna Mwekezaji anavutiwa na eneo lisilo na mali.

    Watu waliposikia British Airways inasitisha huduma, mwezi Machi mwaka huu 2013 wengi walikuwa na mtazamo labda Tanzania uchumi umedorora, SI KWELI!, ni kuwa Waingereza wamesoma alama za nyakati wakajua KASI HII watashindwa kuukabili ushindani kwa Mabingwa watakao kuja ktk sekta ya ndege kutokana na TZ inavyokuwa inagombewa kama mpira wa Kona kwa mali zake kwa sasa, ingawa wao BA wamekaa ktk Soko hili kwa miaka 82 !

    Fedha hupatikana kwenye fedha, na fedha huzaa fedha, mpo hapo?

    Kila mwekezaji anaitafuta Tanzania na yeye apate Mkate wake!

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 01, 2013

    Watanzania hatuelemiki! Swala sio mama ntilie wala biashara kudoda heri mngejua madhara yake msingeandika hayo!Najua walio-comment kutetea wote hawaelewi madhara yake. Kweli sitaingia kula hapo ila kwa faida ya wasiojua ndio mana tunaandika haya. Nenda mkale hayo maKFC mnayotete, kwanza mie siishi Tz.kwa taarifa yenu. Watanzania hatufundishiki...Nendeni mkale hayo makuku na chips zilizokaa kwenye mafriji miaka na zinapikwa in 5 minutes time una chakula tayari. Kazi kwenu wapenda KFC, utamu mdomoni madhara mwilini.

    ReplyDelete
  16. Mi nadhani huyu mzalendo anayepinga KFC, hali chochote! Unadhani vyuma vya kukoboa mahindi vinaishia wapi??? Kama sio kwenye unga na unakula matonge (makubwa makubwa).. Unakula sembe na chembembe za vyuma, hujijui tu... Kila kitu duniani kimeharibika... Waache watu waende na wakati, kama kufa kupo, kupo tu. Siyo makuku ya KFC ndiyo yakuue, sanasana yatakupa shavu tu ndugu yangu......

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...