Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Mheshimiwa Mwantumu Bakari Mahiza kuwa Skauti Mkuu nchini.

Kwa mujibu wa barua ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue  amesema uteuzi wa Mheshimiwa Mahiza umeanza tangu tarehe 19 Aprili, 2013.

Mheshimiwa Mahiza anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Kanali Mstaafu Iddi Kipingu ambaye amemaliza muda wake.

Imetolewa na:

KAIMU KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kila la kheri uihudumie nchi ili vizazi vijavyo waikute sehemu nzuri ya kuanzia

    ReplyDelete
  2. duh jamani kila nafasi anapewa kiongozi aliyepo madarakani,kwa nn wasiwape vijana nafasi hizi ambao bado ni wakakamavu.

    ReplyDelete
  3. Hongera sana Mama Mahiza

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...