Mheshimiwa Angellah Kairuki (MB), Naibu Waziri wa Katiba na Sheria akiwa na mwenyeji wake Mhe. Sayid Ashraful Islam, Waziri wa Serikali za Mitaa, Maendeleo Vijijini na Ushirika, (Wizara inayoshughulika na Usajili wa Vizazi naVifo) wakati wa ziara yake nchini Bangladesh kujifunza namna ambavyo nchi hiyo imeweza kufikia asilimia zaidi ya 95 ya usajili wa Vizazi naVifo.


MheshimiwaAngellah Kairuki,  Naibu akijibu maswaliyawaandishi wa habari wa Bangladesh


Mheshimi wa Angellah Kairuki akifafanua jambo kwa Mhe. Hassanul Haq Inu, Waziri wa Habari wa Bangladesh wakati walipokuwa wakisubiri kukutana na waandishi wa habari wa Bangladesh na kueleza madhumuni ya ujumbe wa Tanzania kwenda nchini Bangladesh kujifunza namna ya kuboresha mfumo wa usajili wa vizazi na vifo hadi kufikia asilimia mia moja (100%).


Mhe. Angellah Kairuki akielezwa jambo na Bw. Nazrul Islam, MtendajiMkuu wa Dhaka South City Corporation



Mhe. Angellah Kairuki akiwa na Sir. Fazle Abed, Mwanzilishi na Mwenyekiti wa taasisi ya BRAC alipotembeleaMakaoMakuuya BRAC.



Mhe. Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wake wa wataalam kutoka Taasisi za RITA, NIDA, TRA, Serikali za Mitaa, e-Government, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Ofisi ya Takwimu,,Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na wenyeji wake.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Yani katika nchi zoote Bangladesh ndio mfano wa kujifunza usajili wa vizazi na vifo!? kazi ipo... Kwanini tusijifunze kutoka kwenye nchi zenye %99-100? kwa nchi kama yetu yenye wastani wa watu milioni 35 na zaidi,ukifanikiwa kuhesabu vizazi na vifo kwa asilimia 95 itamaanisha kwamba watu zaidi ya milioni 1.7 hawatahesabiwa...ili kuleta ufanisi katika shughuli za maendeleo ya jamii, ni lazima vifo na vizazi vyote vihesabiwe, hasa hasa mwelekeo wa vizazi na vifo hivyo; vifo/vizazi kwa mwaka....

    ReplyDelete
  2. Kwa nini Bangladesh? Kwa nini tusijifunze south Africa au marekani? Kwani Bangladesh ndo bora zAidi duniani?

    ReplyDelete
  3. Bangladesh ni nchi masikini kama sisi, isitoshe, wao wana population ya watu milioni 160 and yet wameweza kusajiili vizazi na vifo kwa asilimia 95. Tanzania yenye watu milioni 45, mpaka sasa imesajili asilimia 6 tu. Hivyo kama kuna mahala pa kujifunza Bangladesh ndio more appropriate place to go. Siku zote viongozi wetu wanakosea wanakwenda kujifunza katika nchi zilizoendelea ambako hatulingani rasilimali, teknolojia au ujuZi

    ReplyDelete
  4. Jamani jamani, are we really serious, I cannot comprehend this. Next tutaenda Somalia.

    ReplyDelete
  5. Nadhani ni sawa kwenda kujifunza huko Bangladesh au nchi nyingine. Kwa upande mmoja kuna faid za kwenda huko na hasara pia. Tukiangalia faida ni nchi ndogo (1/6 ya Tanzania)na idadi yake ya watu ni mara nne ya watanzania na pia ni nchi inayoendelea kama Tanzania kwa hiyo uwezo kwa hiyo KUFAHAMU NI JINSI GANI WANAWEZA kukabiliana na changamoto hiyo itasaidia kutumia hizo mbinu hapa tanzania pia..Kama utaenda nchi zilizoendelea utakuta kuwa wanatumia teknologia kubwa hasa alama za viganja na mfumo wa kompyuta ambao kwa sasa ni vigumu kwa serikali yetu kuweza kumudu bajeti yake. Lakini nchi kama Bangladesh wanateknologia ndogo kama sisi tu. Kwa upande mwingine ni kuwa kwenda kujifunza huko ni kama vile tunataka kuendelea na utamaduni wa kutofanya mambo kisasa zaidi kwa kutotumia teknologia ya kisasa kama nchi zilizoendelea ambayo ni HASARA..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...