Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kulia), akikata utepe kuzindua rasmi jukumu la kuwasafirisha Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani kwa Mkoa wa Dodoma. Katikati ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mary Shangali, kushoto ni Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), Dk.Eliezer Feleshi ambao walikuwa katika uzinduzi huo uliofanyika katika Gereza Kuu Isanga Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kushoto) akisalimiana na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mary Shangali baada ya uzinduzi wa mabasi mawili na gari ndogo moja (pick-up). Kushoto Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP), Dk.Eliezer Feleshi. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja, akiwasha moja ya magari yaliyozinduliwa kuashiria uzinduzi wa kuwasafirishia Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi Gerezani kwa Mkoa wa Dodoma. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu Isanga Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba yake kabla ya kuzindua mabasi mawili na gari ndogo moja (pick-up) kwa ajili ya kuwasafirishia mahabusu toka gerezani kwenda mahakamani na kurudi gerezani kwa Mkoa wa Dodoma. Katika hotuba yake mkuu wa jeshi hilo aliwataka maofisa magereza wa mkoa huo wawe makini kuyatunza magari hayo. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Magari matatu ya kuwasafirisha Mahabusu yaliyozinduliwa na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja, katika hafla iliyofanyika Gereza Kuu Isanga Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali-Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Mfanyiwe nini Watanzania hadi mshukuru?

    Tulikuwa hapo nyuma tunashuhudia Makarandinga , yaani Wafungwa na Mahabusi wakisafirishwa kwa Malori.

    Angalieni sasa hadi Mahabusu wanaojumuisha waliosingiziwa, Wahalifu wa kweli na Vibaka wanapanda Mabasi ya kiwango cha ubora wa juu kama haya!

    Makosa hayakosekani ingawa Serikali imejitahidi sana kwa sasa.

    Serikali imeweza mara moja acheni kuibeza na kiutweza!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...