Kijiji cha Ndulamo wilayani Makete kimepewa mradi feki wa maji,ambapo mabomba mapya ya maji hayo yamefunguliwa muda mchache baada ya kuwekwa lakini yote yamefumuka kwa wakati mmoja na kuvijisha maji kama ionekanavyo pichani hapa, uchunguzi nilioufanya umebaiini kuwa mabomba hayo ni feki,yaliyo chini ya kiwango na hayana uwezo wa kupitisha maji mengi na yenye presha kubwa,hadi hivi sasa kijiji hakina maji kwa sababu yamefungwa kwenye chanzo.Mamlaka ya maji inatakiwa kulifuatilia swala hili kwa ukaribu na kufanikisha kutatua tatizo la Maji kijijini hapa.Picha na Edwin Moshi wa Globu ya Jamii,Makete.
Home
Unlabelled
mradi feki wa maji katika kijiji cha Ndulamo wilayani makete
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Hongereni nimeona hata huku ulaya hiyo wanaita drip iligation.
ReplyDeleteNatoa rai kwa watanzania wote wazalendo na nia njema na nchi yetu kutumia blog hii na zingine kwa nia ya 'whistle blowing' kama alivyofanya mtoa taarifa huyu.Tutoe taarifa mapema tunapoona mambo yanafanyika chini ya viwango au kiujanjaujanja katika miradi mbalimbali ili kuepusha hasara kama ya jengo la mtaa wa Indira Ghandi na kufunikwa kwenye machimbo ya kifusi kwa wengi kule Arusha. Mamlaka za usimaimizi na ukaguzi niwazi hazina uwezo au zimelala la sivivyo tusingepata majanga kama haya mfululizo. Tutumie teknolojia tulizonazo kwenye simu kama camera na vinasa sauti ili tuwabambe wachakachuaji zege na wasiojali usalama wa na maisha ya wa Watanzania na kisha turushe na kuwwanika hawa kwenye blog za jamii. Labda hapo wasimamizi na wakaguzi watazinduka. Kama mkaguzi/msimaizi/mshauri wa mradi huu wa maji wialyani Makete angekuwa macho ni wazi mabomba ya kiwango cha chini kama haya yasingetumika. Sasa hapa tukisema mkaguzi/msimaizi/mshauri wa mradiamekula rushwa atalalamika- lakini tusemeje kama kutoka kipyenga kinalia mradi unaanza tu, mambo yanafeli??
ReplyDeleteNatoa rai tena kwa wananchi kutumia blog kama mtoa taarifa huyu tuinusru nchi yetu, uchumi wetu na maisha yetu.
tatizo si mambomba yako chini ya kiwango, bali mafundi ni feki!!!
ReplyDeletewatafuteni wahusika wafikishwe mahakamani au watoe maelezo
ReplyDeleteIrrigation kaka kama umeona ulaya basi wanaita hivi sio iligation
ReplyDeleteSielewi jinsi inaitwa mradi feki. Ianaelekea kuna mtu alibana matumizi na kutumia vifaa finyu! Mkuu wa mradi anastahili kufikishwa kizimbani na ghorof lake liwe mali ya kijiji!
ReplyDelete