wa Mauaji ya Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki parokia ya minara miwili mjini Zanzibar, Omar Mussa Makame (35) kulia akizungumza na mawakili wake Abdalla Juma kushoto na Rajab Abdalla muda mfupi baada ya kutajwa kwa kesi yake Mahakamani hapo.
Mawakili wanaomtetea Mtuhumiwa wa mauaji ya Padri , Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki parokia ya minara miwili mjini Zanzibar, Omar Mussa Makame (35) wakili Abdalla Juma (kulia) na Rajab Abdalla wakiwa mezani pao kabla ya kutajwa kwa kesi ya mteja wao katika mahakama Kuu Vuga mjini Zanzibar
Mtuhumiwa wa Mauaji ya Padri Evarist Mushi wa Kanisa Katoliki parokia ya minara miwili mjini Zanzibar, Omar Mussa Makame (35) akiwa katika Mahakama Kuu ya Zanzibar kabla ya kesi yake kutajwa mahakamani hapo.
Picha zote na Haroub Hussein
KWA MTU KUPOTEZA UHAI, JE KUNA JAMBO LA KUFURAHISHA NA KUMFANYA YEYOTE -WHETHER NI MTUHUMIWA AMA ASIYE MTUHUMIWA- KUTABASAMU NAMNA HII? evil, evil, evil, SHAME ON YOU.
ReplyDeleteTanzania kuna Amani kweli.jamaa hata havalishwi bullet proof akisindikizwa mahamani. na ana bonge la tabasamu Duuh.Waje huku wajione.
ReplyDeleteMdau USA
Jamani nimie peke yangu sijaelewa ama something is seriously wrong with this man? anachocheka ni nini? kuondoa uhai wa mtu yeyote duniani ni a very evil act and for him to seat there and smile as though he won a lottery is beyond me! shame on you! Mungu wako ndo atakaye kuuhukumu.
ReplyDeleteKUNA WATU WANAMAUZI KWELI,NAHIS HAKUTEGEMEWA KUSHIKWA
ReplyDeletehivi huyu ndio anafanana na ile picha iliyochorwa "kitaalamu", nadhani tunahitaji kupima macho.
ReplyDeletekesi ina utata kweli kweli hiyo, muwaji qa kweli yuko nje anakula kuku wacha tuyaone.
ReplyDeleteKwa nini munamuhukumu kwamba yeye ni muuaji wakati hata kesi yenyewe haijaanza?
ReplyDeleteShame on you too!
Siyo tabasamu ya kawaida amechanganyikiwa Hutu kama kweli ni yeye ameua au la.
ReplyDeleteMunaoshangaa jamaa anavyotabasamu mlitaka alie? Kama hajahusika na hayo mauaji?
ReplyDeleteKwanini asiwacheke hao polisi kwa uchungizi mbovu wa kumkamata mtu sio
Tena kwa usumbufu atakaopatiwa na kuitwa muuaji kabla hata ya hukumu kutoka hamuoni ni makosa?
hivi watz wenzangu wapi mwaenda mtu anafanishwa na mtuhumiwa wa mahuaji ya padri tayari mmehukumu tayari kwani tuhuma ni chanzo cha kupata ukweli.
ReplyDeleteNi vizuri tukavuta subira kwakua huyu bado ni mtuhumiwa hakuna haja ya kumlaani kabla hajatiwa hatiani, nadhani picha halisi inaonekana hata yeye mwenyewe hana shaka kua atapangua kikamilifu tuhuma dhidi yake.
ReplyDeleteWatu wapo US wengine UK humu ndani hawajui nini maana ya MUUAJI na MTUHUMIWA,
ReplyDeleteHivi nyie kuna aliemuona huyu kaua,kwa taarifa yenu Mwendesha mashtaka ametupilia mbali ushahidi wa uongo aloutoa kamishna na timu yake yote
na amewambia wamuachie huyu jamaa wakamtafute Muuaji,kwanza masaa 24 yamepita sheria huyu hana kesi hata kama auwe,
Huyu jamaa kilichomponza ni ile kauli yake alipotoa maoni yake katika kongamano la katiba kuwa Watu wakichoka basi wataingiza silaha kupambana,
Polisi wameshindwa kumpata mtu wameona bora wamkamate huyu,Shame on you mlotoa maoni kulinganisha Mtuhumiwa na Muuaji,
he has the right to smile or even laugh because he's innocent until proven guilty. do they have a concrete evidence to connect him with the murder? "no". To be honest, i do not believe evidence based on eye witness, its always not accurate.
ReplyDeleteWatu wengine wapuuzi sana hasa watanzania wanapenda kuchonga sana. Huyu jamaa awe mtuhumiwa au muuaji anacho smile ni nini???? Maoni ya watu wengine hapa yanaonyesha jinsi gani tuna akili finyu. Hata kama wewe sio muuaji kinachokufurahisha ni nini unapotuhumiwa kwa mauaji???
ReplyDeleteTABASAMU LA NGUVU BILA WASIWASI WOWOTE, HADI RAHA ... MTU UKIWA UMESINGIZIWA KESI HAMNA CHA KUOGOPA, ANAYEOGOPA NI YULE MWENYE MAKOSA. KWANZA KESI YENYEWE INAONEKANA ANAUNDIWA TU BAADA YA KUKOSEKANA MHALIFU WA KWELI. POLISI WA BONGO NA FBI WAO WANAONEKANA NI WABABAISHAJI TU.
ReplyDeletehapa ninachokiona ni Watanzania wengi tunakurupuka, hata ukiangalia haya maoni, kwa nini asitabasamu wakati anajuwa kuwa police wamechemsha na ndio maana DPP ameshawarushia jalada lao na kamwambia Kamishna Mussa wakamtafute muuwaji kuwa huyu hahusiki na mauaji ila nyinyi munakurupuka eti alie, alilie nini wakati ana uhakika keshatolewa kwenye orodha ya wauwaji, police wanachokifanya ni kutapatapa tu wakifkiria pressure ya kanisa huku mtuhumiwa hawajampata juu ya kuletea mpaka FBI
ReplyDeleteDuh Maajabu
ReplyDeleteNakupenda Tanzania
ReplyDeletekwa wasiomjuwa, kutabasamu kwa huyu swahiba ndio kawaida yake na ndio maisha yake kama alivyo Kikwete.Undani zaidi mungu ndie ajuwae na ndio atakae muongoza.
ReplyDeletemsimuhukumu mtu asie na hatia kwani bado ni mtuhumiwa. sio kila endae jela wote wana hatia huwa ni wapita njia. kunakutendewa haki ama batili yote ma2 yanawezekana.
Mola amsaidie kijana huyu.kwani situnakumbuka yale ya Lulu dhidi ya kanumba."TUTENDEANE HAKI WANADAMU DUNIA TUNAPITA".Wasia wangu kwenu