Wakati Serikali ikipoteza mabilioni ya Pesa kwa utengenezaji na ukarabati wa barabara kila kona ya nchi, baadhi ya wananchi wachache wa Maeneo ya Kitunda Relini Kona ya Kizuiani kama inavyoonekana katika picha wamekutwa leo wakikata rami na kuaribu barabara na miundombinu kwa ajili ya kupitisha bomba la maji la mtu binafsi.
Swali la kujiuliza Mbunge, diwani, wajumbe na wawakilishi wa Serikali za mitaa mpo wapi?? Nani ameruhusu uharibifu wa miundombinu ya maeneo haya na kwa misingi ipi??
Muheshimiwa Magufuli na wizara yako husika tunaomba ufuatilie ili swala na wanaohusika ktk uharibifu huu wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.
maji ni uhai; bila maji mambo hayaendi. Kwanza wa kulaumiwa ni serikali; haijapeleka huduma ya maji kwa wananchi wake. Wanasema kila kitu kina chanzo chake. Kama wangekuwa na maji na wakaharibu kama wanavyoharibu ungewalaumu; lakini kwa sasa hatuwezi kutoa lawama. Kama unavyojua taabu ya maji ilivyokuwa dar es salaam kwa walala hoi wengi.
ReplyDeleteHao ndio Watanzania walio wengi. Kwa kupiga kelele barabara ikiwa haipitiki utaomba ufe. Sasa Maghufuli akafanye nini wakati mimi na wewe tunaona na kushangaa tuu?
ReplyDeleteBasi mtu kama huyu mwenye hili bomba la maji, na hawa waliokata barabara ili kupitisha bomba la maji utawakuta nao wanailaumu serikali.
ReplyDeleteAlipata kibali cha kupitisha bomba hilo toka kwa M/kiti wa serikali ya Mtaa wa hapo kwake! Ebo! ndo Tz!
ReplyDeleteHAYA SASA
ReplyDelete