Kuna wadau wanataka ngoma hii iwe wimbo wa Taifa. Wadau mnasemaje??

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Ni wimbo mzuri sana. Ninakumbuka wakati huo wa shule ya msingi, tuliupiga sana shuleni wakati mwalimu wa zamu akikaguwa usafi. Ole wako uwe na kucha ndefu au hukuchana kipilipili chako.

    Ukitafakari kwa makini maneno ya wimbo huu mtamu utagunduwa kuwa au ulitungwa na mtu M-TZ aliyekuwa nje ya nchi, au kama alikuwa ndani ya nchi basi wimbo huu walengwa wake ni wa-TZ waliokuwa nje, lakini inawezekana hata wa ndani pia. Angalia kwa makini maneno yaliyomo katika ubeti wa pili na wa tatu, utagunduwa kile ninachojaribu kukiongelea.

    Ni wimbo wenye maneno mazito ya kizalendo,toka kwa mtu aliyeipenda nchi yake, kwa wakati huo. Samahani, sijui kama siku hizi maneno hayo yana maana tena. Kama yana maana basi mimi ninapendekeza yafuatayo.

    Binafsi nadhani wimbo wa Taifa uliopo sasa hivi hauna mapungufu yeyote. Mdundo wake ni safi na maneno yake yanagusa:Wa TZ, Wa-Africa, na pia Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo basi wimbo huu Tanzania Tanzania ingefaa utafutiwe nafasi fulani katika jamii yetu ya WaTZ ili uwe unasikilizwa (unasikika) mara kwa mara. Vinginevyo utapotea.
    Asante kwa kutukumbusha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...