
Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa
Magonjwa ya Binadamu (NIMR) leo imeanza mkutano wake wa 27 wa mwaka kwa
watafiti Wanasayansi jijini Arusha ambapo Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein
anataraji kuufungua rasmi jioni ya leo.
Pamopoja na Mkutano huo wa
NIMR, pia mkutano wa pili wa Wanasansi kuhusiana na Masuala ya Afya barani
Afrika unafanyika sambamba na mkutano huo ambapo watafiti mbalimbali duniani
wanatoa mada juu ya tafiti mbalimbali za magonjwa ya binadamu.
Mkutano huo ambao umebeba
kauli Mbiu ya Mabadiliko ya Mazingira katika Utafiti wa Afya 'Changing landscape in Health Research' utafanyika kwa siku nne
katika Hotel ya Snow Crest jijini Arusha.
Pichani ni Dk. Jeff Waage
kutoka Uingereza akiwasilisha mada juu ya Kilimo na Afya katika Mabadiliko ya
Mazigira katika Utafiti wa Afya.
Baadhi ya washiriki mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania wakifuatilia mada mbalimbali wakati wa mkutano huo jijini Arusha hii leo. Baadhi ya Wabunge nao wamealikwa kushiriki katika mkutano huo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...