Nyumba iko Mwananyamala "B" inatazamana kabisa na ofisi ya Posta. Bei: 
Shilingi za kitanzania Milioni mia moja na Themanin(180,000,000/= ). Kwa maelewano zaidi tafadhali wasiliana na Ndugu Ramadhani Said Sululu kwa namba 0754-380571. Au 0715-380571 Au 0783-380571. 

Karibuni sana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 35 mpaka sasa

  1. Is this real? Ooohhhh no, I cannot believe it, can someone explain to me please?

    ReplyDelete
  2. Unauza nyumba au kiwanja?

    ReplyDelete
  3. Mbona naona nyumba ya mwaka 70 kwenye kiwanja cha Sqm chini ya 250! Hiyo ndo Mil 180!!!!!

    Hata robo ya hiyo sitoi!

    ReplyDelete
  4. nyumba nzuri saana hiyo kwa nini unaiuza?

    ReplyDelete
  5. Ni kweli sio utani,kwa mdau wa kwanza hapo juu nimejaribu kumpigia muhusika! Hapo ni kiwanja ndicho kinachouzwa coz hiyo sio nyumba ya kukaa mtu atakae nunua kwa hizo hela so hapo ni kiwanja ndicho kinachouzwa!!

    ReplyDelete
  6. hiyo nyumba au banda la kuku

    ReplyDelete
  7. Ningeinunua labla kungekuwa hamna kufa,hilo gofu then uswazzzz hivyo aisee ni blaaa

    ReplyDelete
  8. kweli bongo pesa haina thamani!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  9. Mhhh mbona bei ya nyumba haiendani na hadhi ya nyumba yenyewe!!!!!

    ReplyDelete
  10. Hakuna nyumba hapo hata niaibu kuweka picha kama hizo eti kwa gharama ya mamilioni ya shilingi. Iwe nyumba au kiwanja kwa mwonekano huo hakuna kitu hapo

    ReplyDelete
  11. Aseme anauza kiwanja ambacho kitahitaji kusafishwa>

    ReplyDelete
  12. basi ukiona hivyo ndugu wameshindwa kuelewana wameona bora wauze wagawane wako kama 8 hivi na wajukuu humohumo halafu ina kesi mahakamani na wapangaji hawataki kuhama.

    ReplyDelete
  13. That is $111,248.46! See what I can get for less than that in Tampa, Florida http://www.floridamoves.com/property/details/1126163/MLS-U7564778/18960-Duquesne-Dr-Tampa-FL-33647.aspx?SearchID=15378540&RowNum=90&StateID=14&RegionID=0&IsRegularPS=True&IsSold=False

    ReplyDelete
  14. Nadhani thamani ya nyumba hailingani na bei iliyotolewa. Hii ni kama dolla 150,000. Ukienda Marekani au ulaya kwa bei hiyo unapata nyumba nzuri sana zaidi ya hii.

    ReplyDelete
  15. huyu anauza kiwanja kwa hiyo angetakiwa aseme ukubwa wa hicho kiwanja. Bila kujua ukubwa wa kiwanja picha ya hii nyimba haisaidii kitu kulinganisha na hiyo 180 million!

    ReplyDelete
  16. laki moja na themanini au?

    ReplyDelete
  17. Hivi nyumba kama hizo bado ziko Dar,
    kweli mimi sirudi huko afrika, tunaambiwa maendeleo yako ndio hivyo kumbe? jamani nyumba hio iko mji mkuu wa nchi ya tanzania mimi sirudi wala vipi haiwezekani hapo ndio mwananyamala ! kwetu je Lindi kutakuwaje

    ReplyDelete
    Replies
    1. I like my city but ..inasikutisha sana kuona pango kama ilo downtown,
      ilafu na hiyo bei. I thing there r typing
      error* anamaanisha labda 1,800,000.

      Delete
  18. Disgusting!

    ReplyDelete
  19. Dizayni alitaka kusema milioni 1 na laki 8; akakosea akasema milioni 180.

    ReplyDelete
  20. Mie hata bure siitaki

    ReplyDelete
  21. Hiyo ni nini!!!!!!!???????? wacha mambo jamaa yangu! Yaani gharama ya hiki ninachokiona au macho yangu!

    ReplyDelete
  22. Unashangaa nini mnadhani mwanaya B niile ya zamani?hutaki kununua kwabei hioo kanunueni mjini muangukiwe na maghorofaa!mji umebadilikaaa.

    ReplyDelete
  23. hiyo ni karibia dola $116,000.00 ambayo naweza kupata nyumba kwa hapa marekani. Naona watanzania hatuko serious mtu anajipangia bei tu bila kuweka vigezo vya maana. Kwa kuanzia tu hapo ni kiwanja ndio unauza siyo nyumba..

    ReplyDelete
  24. HAHAHAHAHAHAHAHAHHA 180 MILLIONI????. INNALILAH WAINAILYHI RAJIUN

    ReplyDelete
  25. hih hih ihi hi No comment wacha nijichekee na hizo comment humu ndani,bora wengine waulize ni laki na themanini au milioni na laki nane?

    Dah!!!! UK unapata detached za kisasa 2 na unakodisha uko mbali kwa bei hiyo ushajenga ngapi ?

    ReplyDelete
  26. Kushangaa lazima! Mwananyamala napafahamu sana uswahili vile vile! Nina heka moja Kimara na nyumba nilitumia katibia milioni 60 kwa ujenzi na nikilinganisha nashangaa kabisa tuambie basi kiwaja kina ukubwa gani japo hata kwa bure sitaki. Wajinga ndio waliwao

    ReplyDelete
  27. Nafikiri wachangiaji hapo juu hamfahamu Mwan..B ilivyo sasa hivi hapo mahali ni hot cake sasa hivi.

    ReplyDelete
  28. kama hamna hela semeni msianze blablaaa wengine hamrudi bongo wengine uchafu mbona mkisafiri nyinyi kwenda nje mnakuwa hayawani hapa mnanikumbusha yule mtoto aliyekwenda kwa jirani enzi zetu akakuta makochi, mazulia na nyumba nzuri safi wakati ulipofika kurudi kwao mtaa wa pili akagoma na akaanza kulia acheni ujinga kwenu kama kuchafu si mmekimbia kufagia sasa akufagilie nani shuwaini nyie.
    mdau.
    mbagala sokoni.

    ReplyDelete
  29. Wabongo hii ndio ila yenu ya ujinga na ufedhuli. kama hamna uwezo wa kununu basi semeni tu mtanunuliwa mnachotaka. nawengine acheni kupaka matope kwenu kwani mkataa kwao ni mtumwa tu.

    Ankal waweke sawa hawa vibuzi marika.

    ReplyDelete
  30. Jamani asiyejua maana usimwambie maana hiyo nyumba ina hati ipo mjini unaweza kujenga nyumba ya kisasa hata hotel yawezekana. Ni Business Place. Chezea M'nyamala ww!!!!!

    Nendeni mkanunue mabondeni mpate habati zenu.

    ReplyDelete
  31. Basi abomoe kabisa asafishe ndio aanze kutangaza anauza kiwanja! hiyo nyumba hapo haina maana, ya nini?

    ReplyDelete
  32. Hivi !! Naomba niulize ! Kuna vyombo vya kuweza kuhakiki thamani halisi ya projects kama hizi!? Ama ni vile umejisikia tu!!!

    Its hot cake or whatever ni vile mtu unaweigh opportunity!!! Nazungumzia value for money na uhalisia wake....LOL!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  33. Mdau Fred Macha alikuwa amepanga chumba kwenye jumba hili wakati alipotunga kile kibao chake cha PAKA MWEUSI!!!

    ReplyDelete
  34. Kwa bei hiyo ni bora nitumie Tshs. 250,000/= nikanunue Kiwanja cha Shamba Vikindu halafu nitatumia Tshs. 50 Million nikajenga Ghorofa Vikindu huku Tshs. 130 Million zikibaki Benki!


    Zaidi ya hapo ikiwa itagundulika kwa uhakikisho wa Kisayansi labda kama hapo Mwananyamala chini ya nyumba ktk Kiwanja hicho pana Madini kama DHAHABU, ALMASI ama TANZANITE ndio naweza kutoa bei hiyo ya Tshs. 180 Million kununua.

    Tshs. 180 Million ni ndogo ?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...